Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stars yainyoosha Zimbabwe

Muktasari:

  • Sare hiyo imeifanya Taifa Stars isonge mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kushinda bao 1-0 jijini Dar es Salaam na sasa itacheza na Msumbiji katika mechi ya raundi ya pili.

ZIMBABWE.TAIFA Stars imesonga mbele katika mechi za kuwania kufuzu Kombe la Afrika 2015 baada ya jana Jumapili kutoka sare ya mabao 2-2 na Zimbabwe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Harare.

Sare hiyo imeifanya Taifa Stars isonge mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kushinda bao 1-0 jijini Dar es Salaam na sasa itacheza na Msumbiji katika mechi ya raundi ya pili. 

Katika mchezo huo, Zimbabwe ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya tatu lililofungwa na Danny Phiri kwa shuti kali baada ya mabeki wa Taifa Stars kuchelewa kuokoa mpira. Dakika ya 21, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliisawazishia Taifa Stars kwa bao safi la kichwa akiunganisha kona ya Simon Msuva.

Taifa Stars ilipata bao la pili dakika ya 46 mfungaji akiwa Thomas Ulimwengu aliyepokea pasi ndefu ya Oscar Joshua, Zimbabwe ilicharuka baada ya kuingia kwa bao hilo na kusawazisha dakika ya 54 mfungaji akiwa Denver Mukamba kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona.

Lakini kabla ya mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa hapa Harare wakiwa na imani kwamba Zimbabwe yao itafuzu, kulikuwa na matukio  manne tata ambayo Taifa Stars ilikabiliwa nayo kabla haijaingia uwanjani.

1.Chakula cha ovyo

Meneja wa Taifa Stars, Boniface Clemence, aliliambia Mwanaspoti kuwa chakula walichokuwa wakipatia na  wenyeji wao katika Hoteli ya Pandhari waliyowaandali hakikuwa na hadhi.

2.Yaandaliwa chakula cha usiku eneo la wazi

Unaifahamu vizuri baridi ya Harare? Usiombe, ni kali sana hasa nyakati za jioni. Lakini katika hali ya kushangaza  Ijumaa jioni siku ambayo Taifa Stars iliwasili Harare, wahudumu wa Hoteli ya Pandhari waliiandilia chakula chakula cha usiku eneo la wazi lililokuwa na baridi kali.

3.Vyumba Vyafungwa

Huu ulikuwa mkasa wa kushitua zaidi ambao Taifa Stars ilikutana nao katika nchi ya Zimbabwe ambayo kabla ya uhuru wake ilikuwa inafahamika kama Rhodesia ya Kusini.

Sakata lenyewe lilikuwa hivi, Taifa  Stars ilikwenda kufanya mazoezi katika uwanja mzuri iliojitafutia wenyewe wa Shule ya Sekondari ya Heritage.

Baada ya mazoezi kukamilika msafara ulirejea hotelini, lakini ajabu ni kwamba walikuta vyumba vya wachezaji na viongozi vimefungwa na wahudumu wakagoma kuvifungua. Walipoulizwa sababu, wahudumu hao wakasema ni kwa kuwa hoteli inakidai Chama cha Soka Zimbabwe (Zifa).

Hali hiyo ilisababisha wachezaji na viongozi wa Taifa Stars wakae eneo la mapokezi kwa zaidi ya saa moja hadi pale Rais wa TFF, Jamal Malinzi, alipookoa jahazi kwa kulipa Dola 3000 na kufunguliwa.

4. Yazuiwa kuingia uwanjani

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na wenyeji wao Zifa,Taifa Stars ilipangiwa kufanya mazoezi Uwanja wa Taifa juzi Jumamosi kuanzia 9 alasiri.

Lakini ilipofika uwanjani hapo ilizuiwa na walinzi waliodai kwamba kulikuwa kuna kazi maalumu ndani.

Baada ya msafara wa Taifa Stars kuingia kwa nguvu uwanjani hapo, ndipo ilipobainika kwamba wenyeji nao walikuwa wakifanya mazoezi. Lakini wakalazimika kuipisha Stars.