Taifa Stars sasa mguu sawa kambini

Wachezaji wanaotakiwa kuripoti kambini ni :Deo Munishi ‘Dida’, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Muktasari:

KIKOSI cha Taifa Stars kinaingia kambini Jumatatu ijayo tayari kwa safari ya kwenda Gaborone, Botswana kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Afrika 2015 dhidi ya Msumbiji.
Taifa Stars imepanga kuweka kambi ya muda Botswana kisha kurejea nchini kabla ya Julai 20 tayari kwa mchezo wa kwanza wa mtoano na Msumbiji,
Wachezaji wanaotakiwa kuripoti kambini ni :Deo Munishi ‘Dida’, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Harun Chanongo, Himid Mao, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngassa na Mwagane Yeya.
Kikosi hicho kilifanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo baada ya kuitoa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2. Awali Stars ilishinda 1-0 kisha zikatoka 2-2.