Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taifa Stars yapata pigo Morocco

STARS Pict

Muktasari:

  • Mamlaka za uongozi nchini Morocco ilipokuwa kuchezwe mechi hizo mbili za Stars imetangaza kuzuia kuzuia kwa michezo yote ya kimataifa iliyokuwa ifanyike nchini humo kwa hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepata pigo baada ya kufutwa kwa ratiba ya michezo yake ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Uganda na Rwanda kutokana na uwepo wa tishio la ugonjwa wa Ebola.

Mamlaka za uongozi nchini Morocco ilipokuwa kuchezwe mechi hizo mbili za Stars imetangaza kuzuia kuzuia kwa michezo yote ya kimataifa iliyokuwa ifanyike nchini humo kwa hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) ilisema Uganda imefuta mechi zake hizo kutokana na tahadhari ya masuala la Afya.

ZENG 01

Uganda  maarufu kwa jina la 'The Cranes', ilikuwa na mechi mbili za kirafiki dhidi ya Tanzania na Madagascar, ambazo zilikuwa zichezwe jijini Marrakech, nchini Morocco wiki hii.

Hata hivyo, wakati Uganda ikitangaza uamuzi huo, tayari Tanzania na Madagascar, zilikuwa zimeshawasili jijini Marrakech, tayari kwa mechi hizo mbili.

ZENG 03

Uamuzi huo, utaifanya Tanzania kusalia na mchezo mmoja pekee wa kirafiki dhidi ya Rwanda, utakaopigwa Juni 9, baada ya ule wa Juni 5 dhidi ya Uganda kufutwa.

Taarifa zaidi zinasema, uamuzi huo wa Uganda unakuja wakati ambao taifa hilo likikumbwa na kesi za uwepo wa maradhi ya Ebola, ikiripotiwa watu 15 wamekumbwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

Wakala aliyekuwa anasimamia uandaaji wa mchezo huo, amekutana na wakati mgumu juu ya uhakika wa afya kwa wachezaji wa timu hiyo dhidi ya maafisa wa Morocco.