Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachezaji saba Zanzibar wafukuzwa kwa tuhuma za kubeti

KUBETI Pict

Muktasari:

  • Wachezaji hao walibeti katika michezo miwili waliocheza na Malindi pamoja na New City.

Uongozi wa timu ya Junguni United iliyopo Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL) umewafukuza wachezaji saba wa timu hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na michezo ya kubashiri matokeo ya mchezo (betting).

Wachezaji hao walibeti katika michezo miwili waliocheza na Malindi pamoja na New City.

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Junguni, Suleiman Mwidani ambaye amesema, wachezaji hao wamevunja katiba ya klabu hiyo na kukiuka kanuni ya Ligi Kuu ya  Zanzibar ya 2024/25, kifungu namba mbili na tatu, sura ya 23.

"Kulingana na sheria mchezaji hatakiwi kubeti, hivyo wachezaji hao wamefanya kosa hilo na wanapaswa kuchukuliwa hatua," imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, baada ya viongozi kufanya uchunguzi na kujiridhisha wamewasimamisha wachezaji hao kujihusisha na shughuli yoyote inayohusu timu hiyo na kucheza mpira wa miguu.

Pia, viongozi hao waliliomba Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) kuwapa adhabu, ili kukomesha michezo ya bahati nasibu kwa wachezaji wenye nia ya kurudisha maendeleo ya soka kisiwani hapa.

Wachezaji hao saba waliosimamishwa kwa tuhuma hizo ni; Salum Athumani 'Chubi', Ramadhan Ally Omar 'Matuidi', Abdallah Sebastian, Danford Mosses Kaswa, Bakari Athumani 'Jomba Jomba', Rashid Abdalla Njete na Idd Said Karongo.