Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watano wasimamishwa KenGold

Muktasari:

  • KenGold ambayo imeshiriki Ligi Kuu Bara msimu huu kwa mara ya kwanza, imekuwa timu ya kwanza kushuka daraja baada ya kufungwa 2-1 na Coastal Union Jumatatu wiki hii ikibaki na pointi 16 ambazo haziwezi kuwafanya kutoka ndani ya nafasi mbili za chini katika mechi tatu zilizobaki.

TAARIFA zinabainisha kuwa, siku chache baada ya KenGold kushuka daraja, imewasimamisha baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho na kocha wao wa viungo ikidaiwa ni kutokana na sababu za kinidhamu.

KenGold ambayo imeshiriki Ligi Kuu Bara msimu huu kwa mara ya kwanza, imekuwa timu ya kwanza kushuka daraja baada ya kufungwa 2-1 na Coastal Union Jumatatu wiki hii ikibaki na pointi 16 ambazo haziwezi kuwafanya kutoka ndani ya nafasi mbili za chini katika mechi tatu zilizobaki.

Wanaotajwa kusimamishwa ni Seleman Bwenzi, Abdallah Masoud ‘Cabaye’, Steven Duah, James Msuva na Uhuru Seleman ambaye ni kocha wa viungo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Cabaye ambaye ni miongoni mwa waliosimamishwa, amekiri kusimamishwa kwake kumetokana na utovu wa nidhamu.

“Nilipishana kidogo na viongozi kwa sababu ya mambo fulani ambayo ni haki yangu lakini hawakunipatia kwa wakati, hivyo nilichoka kama binadamu ndio tukapishana.

“Kwa sasa nipo nasubiria hatima ni ipi ila nimetii adhabu niliyopewa, lakini kwa upande wa wenzangu waliosimamishwa pia sijajua makosa yao,” alisema kiungo huyo wa zamani wa Azam na KMC.

Mwanaspoti lilipomtafuta Katibu wa KenGold, Benson Mkocha kuzungumzia ishu hiyo, alisema kwa sasa hawezi kusema chochote japokuwa kuna mambo yanaendelea ndani ya klabu yao.

“Kuna mambo ya ndani yanaendelea, lakini siwezi kutoa taarifa yoyote mpaka pale muda utakapofika tutaweka wazi yanayoendelea,” alisema.

KenGold imecheza mechi 27 za Ligi Kuu Bara msimu huu ikishinda tatu, sare saba na kupoteza 17, ikifikisha pointi 16 sawa na nafasi inayoshika katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.