Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili Mchenga Stars kusepa

Mchenga Pict

Muktasari:

  • Mchenga inajiandaa na Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) pamoja na timu nyingine na kwa sasa zinafanya usajili kuimarisha vikosi vyao.

MKURUGENZI wa Ufundi wa Mchenga Stars, Mohamed Yusuph amesema timu hiyo itawakosa nyota wake wawili, Jordan Manang na Steve Oguto wanaojindaa kusepa klabuni hapo.

Mchenga inajiandaa na Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) pamoja na timu nyingine na kwa sasa zinafanya usajili kuimarisha vikosi vyao.

Yusuph aliliambia Mwanaspoti, wachezaji hao wanatarajia kutimkia katika moja kati ya zitakazoshiriki ligi hiyo, lakini wamejipanga kuziba nafasi zao kwa kusajili nyota  kutoka timu nyingine na hivyo kuwatoa wasiwasi mashabiki wa Mchenga.

“Tutaziba nafasi hizo kwa kusajiji pia baadhi ya wachezaji kutoka nje ya nchi na wachezaji hao  tutawatangaza baada ya kuanza mazoezi rasmi," alisema Yusuph na kuongeza kuhusu mazoezi ya timu hiyo wamepanga kuanza Machi mwaka huu katika Uwanja wa Spide chini ya Kocha mkuu, Mariam Kiwelo.

Yusuph aliyewahi kuichezea Savio miaka ya nyuma nafasi ya pointi guard (namba 1) alisema mipango waliyonayo kwa sasa ni kubeba ubingwa wa BDL.

Mchenga Stars ilitolewa na JKT katika hatua ya robo fainali ikifungwa michezo 3-1.

“Kama tulitolewa kwa bahati mbaya na JKT na timu hiyo ikawa bingwa kwa nini na sisi tusichukue,” alihoji Yusuph, huku akiipongeza Kangaroo Insurance Brokers na mwenyekiti wao Ivan Tarimo kwa kuisapoti timu hiyo katika ligi ya mwaka jana.