Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yakomaa kileleni

Beki wa Manchester City,Aleksandar Kolarov(katikati) akifurahia na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la tatu la timu hiyo dhidi ya Swansea katika mechi ya ligi kuu England iliyoipigwa jana jumatano kwenye uwanja wa liberty.Man city ilishinda kwa mabao

3-2.PICHA|MAKTABA

Muktasari:

Mabao ya kiungo Mbrazili Fernandinho, Yaya Toure na Aleksandar Kolarov yalitosha kuitoa kimasomaso timu hiyo inayonolewa na Manuel Pellegrini, wakati Swansea City ilifunga mabao yake kupitia kwa Wilfried Bony.

HII ndio Arsenal bana, utawapenda tu. Ndicho unachoweza kusema baada ya wababe hao kung’ang’ania kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kuichapa Cardiff City mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Emirates jana Jumatano.

Mabao ya dakika za mwisho ya Nicklas Bendtner na Theo Walcott yalitosha kuirejesha Arsenal kwenye kilele cha ligi hiyo baada ya kuporwa kwa muda usukani huo na Manchester City kufuatia ushindi wao wa mapema dhidi ya Swansea City.

Kwenye mchezo huo wa Arsenal, presha ilikuwa kubwa kwa mashabiki wake baada ya Cardiff kuonekana kuwagomea uwanjani kwao kabla ya Bendtner aliyetokea benchi kufunga kwenye dakika 88 na dakika mbili baadaye Walcott kuhitimisha ushindi wa kikosi hicho cha Arsenal na hivyo kufikisha pointi 45 baada ya kushuka dimbani mara 20.

Man City iliyotishia kunasa usukani huo wa ligi kama Arsenal ingeshindwa kuichapa Cardiff, yenyewe iliibuka na ushindi safi mbele ya Swansea City baada ya kuwachapa mabao 3-2 wakiwa nyumbani kwao.

Mabao ya kiungo Mbrazili Fernandinho, Yaya Toure na Aleksandar Kolarov yalitosha kuitoa kimasomaso timu hiyo inayonolewa na Manuel Pellegrini, wakati Swansea City ilifunga mabao yake kupitia kwa Wilfried Bony.

Kwa ushindi huo, Man City inashika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 44.

Chelsea iliendelea kuwasha moto baada ya kuichapa Southampton mabao 3-0 nyumbani kwao na hivyo kuzidi kujiimarisha kwenye nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo. Straika Fernando Torres aliona mwezi baada ya kuifungia Chelsea bao la kuongoza katika dakika 60, kabla ya viungo Willian na Oscar kuongeza mengine yaliyomfanya Jose Mourinho na kikosi chake kuzoa pointi zote tatu.

Straika kinara wa kupachika mabao kwenye ligi hiyo, Luis Suarez aliendelea kuwatesa makipa baada ya kufunga bao lake la 20, wakati Liverpool ilipoichapa Hull City mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Anfield.

Bao la kwanza la wababe hao wanaonolewa na Brendan Rodgers lilifungwa na beki wa kati, Daniel Agger.

Michezo mingine ya ligi hiyo, Crystal Palace ilitoshana nguvu na Norwich City baada ya kufungana bao 1-1, wakati Fulham ilipambana kutokea nyuma kuichapa West Ham United mabao 2 - 1.

Eveton imegoma kutoka kwenye tano bora ya ligi hiyo baada ya kuisawazishia Stoke City na hivyo kuambulia sare ya bao 1-1. Mkwaju wa penalti uliopigwa na Leighton Baines ulitosha kuipa pointi muhimu ya ugenini Everton kwenye mechi hiyo wakati wenyeji wao Stoke City walitangulia kwa bao la Oussama Assaidi.

Sunderland ilikuwa hovyo nyumbani baada ya kuchapwa 1-0 na Aston Villa, wakati West Bromwich Albion walizidi kuitibua Newcastle United kwa kipigo cha pili mfululizo baada ya ushindi wao wa bao 1- 0, shukrani kwa bao la penalti na Saido Berahino, huku Mathieu Debuchy akiambulia kadi nyekundu.

Mashabiki waliofurika Emirates, walimshuhudia straika wa zamani wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, ambaye kwa sasa ni kocha wa Molde, alikuwa ameketi na mmiliki Cardiff City, Vincent Tan jukwaani kuitazama timu hiyo kabla ya kufanya mazungumzo ya kuinoa timu hiyo ya Wales.

Tan alimfuata Solskjaer kwa ndege binafsi nchini Norway kwa ajili ya kwenda kuitazama mechi hiyo dhidi ya Arsenal na kisha kufanya mazungumzo ya kumpa kibarua.