Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ancelotti, Brazil mambo yameiva

ANCELOTTI Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa tayari, wawakilishi wa Brazil wapo jijini Madrid kwa ajili ya mazungumzo zaidi na wamepata nguvu zaidi baada ya Madrid kukosa taji la Copa del Rey wakiamini itazidisha asilimia za timu hiyo kuachana na Ancelotti.

MADRID, HISPANIA: SHIRIKISHO la soka la Brazil linaripotiwa kuwa na imani kubwa ya kumpata kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti kuelekea michuano ya Kombe la Dunia kwa Klabu.

Inaelezwa tayari, wawakilishi wa Brazil wapo jijini Madrid kwa ajili ya mazungumzo zaidi na wamepata nguvu zaidi baada ya Madrid kukosa taji la Copa del Rey wakiamini itazidisha asilimia za timu hiyo kuachana na Ancelotti.

Awali, ilielezwa, kocha huyo wa zamani wa AC Milan na Chelsea alikuwa akiangalia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa atafanya vizuri lakini mambo yalikuwa mabaya baada ya kutolewa robo fainali na Arsenal.

Mambo yamekuwa mabaya zaidi baada ya kukosa na Copa del Rey mbele ya wapinzani wao Barcelona hali inayowafanya kuwa katika hatari ya kumaliza msimu bila taji lolote kwani hata La Liga pia wako nafasi yapili.

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano,  Shirikisho la Brazil, lina imani kubwa juu ya kumpata Ancelotti kama kocha mkuu mpya na atajiunga kabla ya Kombe la Dunia la Klabu.

Kama Ancelotti ataondoka inadaiwa huenda Madrid akapewa Jurgen Klopp badala ya Xabi Alonso.

Klopp, 57, aliteuliwa kuwa kiongozi wa masuala ya soka  wa kampuni ya Red Bull miezi michache baada ya kuondoka Liverpool 2024.

Hata hivyo, Klopp anadaiwa kuwa hana furaha katika nafasi hiyo.

Ancelotti alizungumzia ishu yake ya kuondoka Real Madrid wiki iliyopita, akisisitiza kuwa bado yupo katika kipindi cha ‘honeymoon’ akifurahia maisha katika mji huo  mkuu wa Hispania.

 “Nashukuru kuwa hapa Madrid na natumaini nitaendelea kuwa hapa kwa muda mrefu iwezekanavyo.  Kuna presha kweli, lakini hiyo daima huwa inatokea wakati kama  huu.”