Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arne Slot anaishi ndoto za Ancelotti

Muktasari:

  • Baada ya Brendan Rodgers kufutwa kazi Oktoba 2015, Ancelotti aliripotiwa kuwa na mazungumzo kwa ajili ya kuwa kocha mpya, lakini timu hiyo ilamua kumchukua Jurgen Klopp.

MADRID, HISPANIA: NDIO. Kocha wa Liverpool, Arne Slot anaishi ndoto za kocha wa Real  Madrid, Carlo Ancelotti ambaye amekiri kwamba kuifundisha Liverpool ni ndoto yake ya muda mrefu.

Baada ya Brendan Rodgers kufutwa kazi Oktoba 2015, Ancelotti aliripotiwa kuwa na mazungumzo kwa ajili ya kuwa kocha mpya, lakini timu hiyo ilamua kumchukua Jurgen Klopp.

Muda mfupi baada ya kukosa dili hilo, Ancelotti alikubali kuchukua nafasi ya Pep Guardiola huko Bayern Munich, kazi ambayo aliianza mwishoni mwa msimu wa 2015-16.

Ingawa hakupata nafasi ya kuifundisha Liverpool, Ancelotti aliwasili Mrseyside 2019 alipokuwa kocha wa Everton.

Akizungumza na mwandishi wa habari kutoka Italia, Armando Ceroni kupitia kituo cha RSI, kocha huyo mkongwe alisema: “Ndoto yangu ilikuwa kuifundisha Liverpool, lakini nilijikuta Everton na nikaonja ladha ya  ushindani mkubwa uliopo kati yao. Kwa sasa ni shabiki kamili wa Everton. Nilipenda mazingira yao. Kuna mapenzi ya kweli kutoka kwa mashabiki wao. Pia unaona wanavyoumia wakipoteza mbele ya  Liverpool.”

Kocha huyo wa Real Madrid pia alieleza kuwa alikataa nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya Italia 2018 kabla ya Roberto Mancini kuteuliwa kuifundisha.

Alisema: “Nilikataa kuifundisha timu ya taifa ya Italia kwa sababu sikuwa na hamasa ya kufanya hivyo. Ninapenda kuwa uwanjani kila siku nikijiandaa kwa mazoezi. Kuifundisha timu ya taifa kwangu ilionekana kama kazi ya muda mfupi ambayo inanipunguzia ule msisimko wa kila siku.”

Mkataba wa Ancelotti na Real Madrid unamalizika mwakani, lakini safari yake inaonekana kuwa huenda ikatamatika mwisho wa msimu huu ambapo anahusishwa kwenda kuifundisha timu ya taifa ya Brazil wakati Madrid ikitajwa kumtaka kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso.