Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kuzipiku Man United, Chelsea

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Msimu uliopita, Arsenal yenye maskani yake kaskazini mwa London ilikuwa na rekodi ya mapato Pauni 616 milioni, huku mapato yaliyotokana na viingilio na uuzaji wa wachezaji ikizidi kwa Pauni 150 milioni ikilinganishwa na msimu uliopita.

LONDON, ENGLAND: INAELEZWA Arsenal watakuwa na nafasi ya kutumia pesa nyingi zaidi kuliko Manchester United na Chelsea kutokana na faida kubwa ya kufika kwao nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Msimu uliopita, Arsenal yenye maskani yake kaskazini mwa London ilikuwa na rekodi ya mapato Pauni 616 milioni, huku mapato yaliyotokana na viingilio na uuzaji wa wachezaji ikizidi kwa Pauni 150 milioni ikilinganishwa na msimu uliopita.

Inaelezwa faida hiyo ambayo pia itaongezeka msimu huu kwa kufika nusu fainali, inawaweka Gunners katika nafasi nzuri kwenye sheria za usawa wa matumizi ya kifedha, hivyo watakuwa na nafasi ya kutumia zaidi ukilinganisha na wapinzani wao wanaopambana nao katika kuwania wachezaji mbalimbali ambao ni Man United na Chelsea.

Faida hii inaweza kuwapa Arsenal nafasi kubwa zaidi ya kumpata straika Viktor Gyokeres au Benjamin Sesko ambao pia wanawindwa na Man United na Chelsea, ambao huenda wasiweze kupambana katika vita ya pesa kutokana na kubanwa na sheria.

Uwezo wa Man United kusajili wachezaji katika dirisha lijalo utategemea sana na kufuzu Ligi ya Mabingwa kwa kuchukua ubingwa wa Europa League, pia itategemea na kuuza baadhi ya wachezaji.

Kwa sasa timu hii inashika nafasi ya 15 ikiwa chini ya nafasi 10 za juu jambo ambalo litapunguza mapato katika mgao wao wa fedha za udhamini za ligi.

Chelsea wako katika hali ngumu zaidi. Klabu hii imejaribu kwenda sawa na kanuni za kifedha kwa kuuza timu yao ya wanawake na hoteli mbili za Stamford Bridge kwa kampuni yao mama, lakini UEFA imekataa kukubali makubaliano hayo.