Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal mpo? wale jamaa wanacheza

Muktasari:

  • Masupastaa Antonio Rudiger na Kylian Mbappe wamekumbana na adhabu ya kufungiwa mechi moja na kupigwa faini, wakati Dani Ceballos amekumbana tu na kupigwa faini.

MADRID, HISPANIA: NDIYO hivyo. Hakuna mchezaji yeyote kati ya wanne wa Real Madrid waliokuwa wakichunguzwa na UEFA ambaye atakosa mechi ijayo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal, Jumanne.

Masupastaa Antonio Rudiger na Kylian Mbappe wamekumbana na adhabu ya kufungiwa mechi moja na kupigwa faini, wakati Dani Ceballos amekumbana tu na kupigwa faini.

Rudiger alichunguzwa na Uefa baada ya kuwaonyesha mashabiki wa Atletico Madrid ishara ya kuchinja mwezi uliopita kwenye mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Staa wa Kibrazili, Vinicius Junior naye alikuwamo kwenye uchunguzi huo wa Uefa, lakini hakukumbana na adhabu yoyote.

Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya Arsenal kuikaribisha Los Blancos uwanjani Emirates kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uefa ilithibitisha adhabu kwa wachezaji hao wa Real Madrid.

Rudiger na Mbappe kila mmoja atatumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja na faini ya Pauni 34,000 na Pauni 25,000 mtawalia. Ceballos, ambaye aliwahi kuichezea Arsenal kwa mkopo kuanzia 2019 hadi 2021, ametozwa faini ya Pauni 17,000. Na ilielezwa kwamba hakuna hatua zozote za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi ya Vinicius.

Rudiger na Mbappe adhabu yao hiyo ya kufungiwa mechi moja wanatakiwa kuifanya ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Kwa maana hiyo, wachezaji hao wote wanne watakuwapo katika kikosi cha Carlo Ancelotti, wakati mabingwa hao mara 16 wa Ulaya watakapokuwa kwenye vita ya kutetea taji la Ligi ya Mabingwa uwanjani Emirates na ile mechi ya marudiano itakayochezwa Bernabeu, Aprili 16.

Hata hivyo, kocha Ancelotti hatakuwa na huduma ya kipa wake namba moja, Thibaut Courtois kwenye mechi hiyo ya Emirates. Kipa huyo Mbelgiji amekosa mechi tatu kati ya tano za mwisho za Real Madrid katika michuano yote kutokana na kuwa majeruhi, ikiwamo mechi mbili zilizopita baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa.

Kipa namba mbili, Andriy Lunin, naye pia yupo kwenye hatihati kutokana na kuumia kwenye mechi ya Valencia, Jumamosi iliyopita. Kipa namba tatu, Fran Gonzalez, 19, amewekwa tayari, lakini kocha Ancelotti anaamini Courtois atakuwa fiti kwa ajili ya kipute cha Arsenal kitakachofanyika London Kaskazini, Jumanne.

"Courtois anaendelea vizuri, tunafikiri ataweza kucheza Jumanne," alisema Ancelotti, Ijumaa iliyopita.




...