Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal v Madrid, Bayern v Inter usiku wa hesabu kali

Muktasari:

  • Leo, Jumanne itapigwa michezo miwili na mbali na mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 4:00 usiku, mwingine ni katika Uwanja wa Allianz Arena na utazihusisha Bayern Munich na Inter Milan muda kama huo ikiwa ni michezo ya mkondo wa kwanza.

LONDON, ENGLAND: ROBO fainali za kwanza za Ligi ya Mabingwa Ulaya zinapigwa leo na kesho huku macho na masikio yakiwa pale kwenye Uwanja wa Emirate, Arsenal itakapoikaribisha Mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo mikubwa, Real Madrid.

Leo, Jumanne itapigwa michezo miwili na mbali na mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 4:00 usiku, mwingine ni katika Uwanja wa Allianz Arena na utazihusisha Bayern Munich na Inter Milan muda kama huo ikiwa ni michezo ya mkondo wa kwanza.

Arsenal inakutana na Madrid kwa mara ya tatu na mara ya mwisho ni msimu wa 2005/06 katika hatua ya 16 bora  na washika mitutu hao walishinda bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza kisha mechi ya pili iliyopigwa Emirates ikamalizika kwa sare ya 0-0.

Vijana hawa wa Kocha Mikel Arteta wanaingia katika mechi hiyo wakiwa na idadi kubwa ya majeruhi jambo linalozidi kuzua hofu kwao.

Riccardo Calafiori, Gabriel Magalhaes, Kai Havertz, Takehiro Tomiyasu na Gabriel Jesus ni miongoni mwa wachezaji wanaosumbuliwa na majeraha katika kikosi hicho.

Lakini kocha Arteta inadaiwa ameshapata dawa ya kutumia kuhakikisha anafukia mashimo ya mastaa ambao wanasumbuliwa na majeraha.

Kwanza kama kawaida eneo la langoni ni kipa  David Raya, kisha Thomas Partey anaweza kucheza kama beki wa kulia  badala ya Timber na White, hili ni eneo ambalo kiungo huyu ameshawahi kucheza.

Katika eneo la beki wa kati ambapo Gabriel ameumia kuna uwezekano akamtumia Jakub Kiwior acheze pacha na William Saliba. 

Uwepo wa Partey kwenye eneo la ulinzi unaweza kumfanya Mikel Merino kurudi katikati ya uwanja kucheza kama kiungo katikati ya Declan Rice na Martin Odegaard.

Mbadala mwingine wa kuziba la eneo la kati ingekuwa ni kwa Kieran Tierney kuingia kwenye kikosi akaenda kucheza eneo la beki wa kushoto kisha Myles Lewis-Skelly apanda kucheza katikati ya uwanja. 

Ikiwa Arteta atachagua kumrudisha Merino kwenye eneo la kiungo ambalo ni asili yake, Leandro Trossard anaweza kuingizwa kikosini kisha akacheza kama mshambuliaji wa kati, pembeni akisaidiwa na Bukayo Saka pamoja na  Gabriel Martinelli.

Madrid ambayo inashika nafasi yapili katika msimamo wa La Liga ikiwa nyuma ya Barcelona kwa tofauti ya pointi nne, imekuwa haina matokeo mazuri hivi karibuni na mchezo wao wa mwisho ilikubali kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Valencia.

Mchezo wa Bayern Munich na Inter Milan utakuwa unazikutanisha timu hizi kwa mara ya nane na mara yamwisho ilikuwa msimu wa 2022/23 na walicheza mechi za hatua ya makundi na Bayern ikashinda zote.

Kijumla Bayern ambayo ina mataji sita ya michuano hii ndiyo imeshinda mara nyingi (mara nne) katika mechi ilizoikutanisha timu hizi, wakati Inter ambayo ina mataji matatu imeshinda mechi mbili na mmoja ukamalizika kwa sare katika saba zilizopita.

Bayern itaingia ikiwa na pigo la kumkosa staa wao Jamal Musiala ambaye atakuwa nje kwa wiki nane kutokana na jeraha la nyama ya paja.

Mechi nyingine zinatarajiwa kupigwa kesho na Barcelona itaikaribisha Borussia Dortmund wakati PSG ikiwa mwenyeji wa Aston Villa. Mechi zote zitapigwa saa 4:00 usiku.