Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona hali si shwari, Flick akuna kichwa

FLICK Pict

Muktasari:

  • Katika mchezo dhidi ya Celta Vigo, Barca walirudi kutokea nyuma walipokuwa wakiongozwa kwa mabaoa 3-1 hadi kufikia dakika ya 60 na mwisho kushinda 4-3 huku Dani Olmo na Raphinha wote wakifunga mabao mawili mawili.

BARCELONA, HISPANIA: LICHA ya kukaribia kushinda taji la La Liga msimu huu baada ya kushinda mabao 4-3 dhidi ya Celta Vigo, Jumamosi iliyopita, Kocha wa Barcelona, Hansi Flick anakabiliwa na hali ya wasiwasi inayoendelea kuongezeka katika chumba cha kubadilishia nguo cha Barcelona, huku wachezaji watatu wakiripotiwa kushindwa kuficha hasira zao kutokana na kutopata muda wa kucheza.

Katika mchezo dhidi ya Celta Vigo, Barca walirudi kutokea nyuma walipokuwa wakiongozwa kwa mabaoa 3-1 hadi kufikia dakika ya 60 na mwisho kushinda 4-3 huku Dani Olmo na Raphinha wote wakifunga mabao mawili mawili.

Yalikuwa ni matokeo muhimu katika mbio za ubingwa, lakini vyombo kadhaa vya habari vimeripoti kuwa maamuzi ya Flick wakati wa mchezo hayakukubalika kwa baadhi ya wachezaji wa kikosi chake.

Mundo Deportivo iliripoti kuwa mchezaji wa kwanza ambaye alikuwa na hasira kwenye mechi hiyo ni Ansu Fati.

 Winga huyo kijana, ambaye hivi karibuni alipata nafasi ya kucheza baada ya kukaa benchi kwa muda mrefu, alionekana akifanya mazoezi pembeni kabla ya kurejeshwa benchi bila kuingia uwanjani.

Aliporudi kwenye kiti chake, Fati alikanyaga deli la kuwekea vinywaji  kwa hasira, akatupa bibs yake chini na kupiga kitu kingine kwa hasira, akionyesha kutoridhishwa na kutoingizwa kwenye mechi hiyo ambayo ingekuwa ya 10 kwake katika mashindano yote msimu huu.

Dakika ya 60, muda mfupi kabla ya bao la tatu la Celta Vigo, tovuti nyingine iitwayo  SPORT iliripoti Ferran Torres alikasirishwa na uamuzi wa kutolewa uwanjani. Kama ilivyokuwa kwa Fati, Ferran alipiga chupa ya maji kwa hasira na hakumsalimia Flick alipokuwa akitoka.

Mambo hayakuishia hapo kwa Flick kwani, baada ya filimbi ya mwisho, beki wa kulia kijana Hector Fort alionekana ana hasira. Mchezaji huyo, 18, ambaye amecheza mechi 14 tu zenye jumla ya dakika 408 msimu huu, alikataa kumsalimia kocha wake.