Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Brazil 2014: Kufa au kupona England inapokutana na Uruguay leo

Mshambuliaji Wayne Rooney akiwa katika mazoezi na kikosi cha Uingereza hivi karibuni. Picha na AFP

Muktasari:

Timu hizo zinakutana mjini Sao Paulo huku kila moja ikisaka ushindi wake wa kwanza wa Kundi D baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mechi zao za kwanza, Uruguay ililala kwa mabao 3-1 mbele ya Costa Rica na England ilifungwa na Italia 2-1.

NAHODHA wa Uruguay, Diego Lugano amesema kwamba mechi yao ya leo Alhamisi dhidi ya England inatoa picha ya kufa na kupona kwa timu hizo kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Brazil.

Timu hizo zinakutana mjini Sao Paulo huku kila moja ikisaka ushindi wake wa kwanza wa Kundi D baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mechi zao za kwanza, Uruguay ililala kwa mabao 3-1 mbele ya Costa Rica na England ilifungwa na Italia 2-1.

Lugano ambaye pia ni beki wa kati alisema: “Kwa sasa tuko pamoja kwa mara nyingine, imani yetu iko sawa, hatutakiwi kubweteka.

“Tunahitaji ushindi ili tuweze kusonga mbele, na England nao ni hivyo hivyo,’’ alisisitiza.

Kocha wa Uruguay, Oscar Tabarez alisema: “Ni lazima tuendelee kufurahia mashindano, kimsingi mechi haiwezi kuwa rahisi ni lazima tuhakikishe tunakuwa bora.

Ni dhahiri kwamba Lugano anaelewa madhara ambayo England inaweza kuisababishia timu yake hasa baada ya kucheza soka katika Ligi Kuu England msimu uliopita akiwa na West Bromwich Albion.

“Wachezaji wa England wana kasi na nguvu, hiyo maana yake ni kwamba mabeki watakuwa na kazi kubwa,’’ alisema beki huyo mwenye umri wa miaka 33.

Mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez hakucheza katika mechi na Costa Rica licha ya madai kwamba alipona tatizo la goti lakini huenda akaivaa England na amenukuliwa akisema kwamba anajiona yuko njema asilimia 100 kwa ajili ya mechi ya leo.

“Tunatumaini Luis atacheza lakini kama sivyo ni jukumu la sisi wengine kufanya kazi,’’ alisema Lugano huku kocha wake akisisitiza kwamba mechi itakuwa ngumu lakini hakuna lisilowezekana.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Uruguay, kocha wa England, Roy Hodgson anatarajia kumpanga Wayne Rooney nafasi ya kati ya ushambuliaji ambayo mchezaji huyo anaipenda hasa baada ya kushutumiwa kucheza chini ya kiwango katika mechi na Italia.

Rooney alipangwa safu ya ushambuliaji lakini upande wa kushoto kutokuwa msaada katika timu.

Rooney hajawahi kufunga bao katika fainali za Kombe la Dunia na shutuma zinazoelekezwa kwake zinamtia hofu kocha wake ambaye anaamini huenda zikaathiri kiwango cha mchezaji huyo wakati huu ambao England inapambana kufikia hatua ya pili.

Katika mazoezi ya juzi Jumanne, Rooney na Sturridge walipangwa pamoja wakati Raheem Sterling ambaye alianza katika mechi dhidi ya Italia alipangwa na Danny Welbeck.

Katika mechi ya Kundi C itakayochezwa leo, mwamuzi Howard Webb atachezesha mechi kati ya Colombia na Ivory Coast.