Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BRAZIL NOMA: Kazi ipo leo; Hispania v Uholanzi, Fabregas naye rasmi Chelsea

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Brazil wakishangilia ushindi dhidi ya Croatia katika mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia.

Muktasari:

  • Brazil ambao ni wenyeji wa fainali hizo za Kombe la Dunia za mwaka huu, waliduwazwa kwa bao la mapema la kujifunga la Marcelo kwenye dakika ya 11, kabla ya Neymar kusawazisha katika dakika 29 kwa shuti kali la chinichini la guu la kushoto kabla ya kufunga la pili kwa mkwaju wa penalti katika dakika 71.

SALVADOR, BRAZIL

NEYMAR ni habari nyingine. Ndiyo hivyo baada ya staa huyo kufunga mara mbili kuisaidia Brazil kuanza kampeni ya kusaka taji la sita la Kombe la Dunia kwa kuichapa Croatia 3-1 kwenye mchezo wa ufunguzi wa fainali hizo uliofanyika usiku wa jana Alhamisi.

Brazil ambao ni wenyeji wa fainali hizo za Kombe la Dunia za mwaka huu, waliduwazwa kwa bao la mapema la kujifunga la Marcelo kwenye dakika ya 11, kabla ya Neymar kusawazisha katika dakika 29 kwa shuti kali la chinichini la guu la kushoto kabla ya kufunga la pili kwa mkwaju wa penalti katika dakika 71.

Wakati Croatia wakihaha kutaka kusawazisha, walijikuta wakiadhibiwa na kiungo Oscar aliyefunga bao maridadi lililoihakikishia Brazil ushindi baada ya kukimbia na mpira kutoka katikati ya uwanja. Oscar alikuwa kwenye ubora mkubwa sana akihusika kwenye mabo yote ya Brazil.

Hata hivyo Neymar baadaye alitolewa na nafasi yake kuingia Ramires. Ushindi huo unawafanya Brazil kuwa na mwanzo mzuri ambapo kwenye kundi hilo wapo pia Cameroon na Mexico.

Mikikimikiki hiyo itaendelea leo Ijumaa kwa mechi ya nguvu sana kati ya mabingwa watetezi, Hispania watakaokuwa na shughuli mbele ya Uholanzi mechi ambayo inakumbusha  fainali ya mwaka 2010 huko Afrika Kusini.

Ni mechi ambayo inatajwa kuwa nafasi ya Uholanzi kulipa kisasi baada ya kuangukia pua mwaka 2010.

Bao la Andres Iniesta dakika nne kabla ya dakika 30 za nyongeza kumalizika liliiwezesha Hispania kutwaa taji hilo na ikiwa miaka minne imepita wababe hao wanakutana katika mechi ya Kundi B kwenye Uwanja wa Fonte Nova uliopo Salvador.

Baada ya hapo wakali wa Marekani Kusini, Chile watakabiliana na Australia mechi ambazo zitatoa picha ya mwelekeo wa Kundi B.

Nahodha wa Uholanzi, Robin van Persie na wakali wenzake, Arjen Robben, Wesley Sneijder, Nigel De Jong na Dirk Kuyt ni wachezaji watano waliokuwamo katika kikosi cha Uholanzi cha mwaka 2010 ambao pamoja na wenzao wameelezea shauku yao ya kulipa kisasi.

“Ilikuwa ni nafasi yetu kutwaa Kombe la Dunia na kwa hakika tulikuwa karibu mno na hilo,’’ alisema Ron Vlaar ambaye pia ni beki wa Aston Villa.

“Wakati wote kunakuwa na kitu kinachotuhamasisha kufanya jambo vizuri. Kucheza dhidi yao katika mechi ya kwanza ni changamoto kubwa.’’

Kiungo mkongwe, Wesley Sneijder ambaye leo atakuwa anacheza mechi yake ya 100 alisema kwamba jeraha la kufungwa 2010 bado linawaandama.

“Ni kama kovu ambalo bado halijapona, wakati wote linanipa huzuni ninapofikiria,’’ alisema nyota huyo wa Galatasaray.

Hispania chini ya kocha, Vicente del Bosque itakuwa ikiwania kuwa katika kundi moja na Brazil na Italia ambao wameweza kutwaa taji la dunia mara mbili mfululizo.

Del Bosque anatarajia kufanya mabadiliko ya mchezaji mmoja tu katika kikosi kilichotwaa Kombe la Ulaya 2012 ‘Euro 2012’ ambako beki wa Chelsea, Cesar Azpilicueta atachukua nafasi ya Alvaro Arbeloa katika beki ya kulia.

Cesc Fabregas ataanza mbele wakati mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa akitarajiwa kuanzia benchi na kuingia kipindi cha pili.

Van Persie anatarajia kuwa fiti licha ya kuwasili Brazil akiwa ni mmoja wa wachezaji walioibua hofu baada ya kuumia katika mechi ya kirafiki dhidi ya Wales ambayo Uholanzi iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kocha Louis van Gaal anatarajia kuutumia fomesheni ya 5-3-2 nia ikiwa ni kudhibiti mashambulizi ya Hispania na kutengeneza mashambulizi ya kushitukiza.

Wakati huo huo kiungo Mhispaniola, Fabregas amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea Chelsea ambayo itakuwa inamlipa pauni 150,000 kwa wiki.

Usajili huo unatajwa kuwa pigo kubwa sana kwa Arsenal ambayo ilikuwa ikitaka kumsajili tena mchezaji huyo, lakini mwenyewe ameamua kutua Chelsea.