Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea moto, Arsenal balaa

Muktasari:

Mechi hiyo iliyofanyika Carrow Road, Chelsea ilitangulia kwa bao la dakika ya tatu ya mchezo lililofungwa na Oscar baada ya pasi ya Demba Ba, lakini wenyeji walisawazisha kipindi cha pili kwa bao la kichwa la Anthony Pilkington.

MABAO mawili ya ‘chapchap’ katika dakika 10 za mwisho yaliyofungwa na Eden Hazard na Willian yalitosha kwa Chelsea kuisambaratisha Norwich City mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu England, jana Jumapili.

Mechi hiyo iliyofanyika Carrow Road, Chelsea ilitangulia kwa bao la dakika ya tatu ya mchezo lililofungwa na Oscar baada ya pasi ya Demba Ba, lakini wenyeji walisawazisha kipindi cha pili kwa bao la kichwa la Anthony Pilkington.

Lakini wachezaji walioanzia benchi Hazard na Willian waliingia kumpa kocha Jose Mourinho ushindi wake wa kwanza nje ya Stamford Bridge kwenye Ligi Kuu baada ya kufunga mabao hayo mawili ndani ya dakika 10 za mwisho.

Nayo Arsenal ilibanwa na West Bromwich Albion kwa sare ya bao 1-1.

West Brom ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 41 lililofungwa na Claudio Yacob kwa pasi ya Morgan Amalfitano.

Jack Wilshere alisawazisha bao hilo dakika ya 62 kwa shuti la mguu wa kushoto akiitumia vizuri pasi ya Tomas Rosicky.

Kwenye mchezo mwingine wa ligi hiyo, Southampton waliinyuka Swansea City mabao 2-0 kwenye Uwanja wa St Mary’s, shukrani kwa mabao ya Adam Lallana na Jay Rodriguez, wakati Tottenham ililala kwa mabao 3-0 mbele ya West Ham.