Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristiano Ronaldo bado tishio kwa utajiri

CR Pict
CR Pict

Muktasari:

  • Sio namba tu hata upande wa fedha, Cristiano Ronaldo bado anakimbiza baada ya kushika namba moja kwa mara ya pili mfululizo katika orodha ya wanamichezo wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani.

Mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo ameendela kuwaburuza wanamichezo akiongoza katika orodha ya wanamichezo 100 wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa mwaka 2024, baada ya kuingiza Pauni 205 milioni (zaidi ya Sh 650 bilioni).

Kwa mujibu wa ripoti ya Forbes, Ronaldo, ameingiza kiasi hicho kupitia mshahara wa Pauni milioni 168 na Pauni milioni 50 kutoka kwa mikataba ya matangazo na makampuni kama Nike, Herbalife na Armani.

Jon Rahm mcheza golf anashikilia nafasi ya pili kwa Pauni 172 milioni, huku Lionel Messi, anayekipiga Inter Miami, akishika nafasi ya tatu Pauni 107 milioni.

Wachezaji wengine wa soka walioingia katika orodha ya wanamichezo 10 bora wanaolipwa zaidi ni Kylian Mbappé (Pauni 87 milioni), Neymar (Pauni 85 milioni) na Karim Benzema (Pauni 84 milioni).

Kwa upande wa ndondi, Tyson Fury ameorodheshwa katika nafasi ya 64 akikusanya Pauni 31.7 milioni.

Kilichowashtua wengi ni kuwa katika orodha hiyo wa mastaa 100 mwaka huu, hakuna mwanamichezo wa kike aliyeingia katika orodha hiyo.


10 bora hii hapa;

1.        Cristiano Ronaldo (Mpira wa miguu): Pauni 205 milioni

2.        Jon Rahm (Golf):  Pauni 172 milioni

3.        Lionel Messi (Mpira wa miguu): Pauni 107 milioni

4.        LeBron James (Kikapu):  Pauni 101 milioni

5.        Giannis Antetokounmpo (Kikapu): Pauni 88 milioni

6.        Kylian Mbappé (Mpira wa miguu): Pauni 87 milioni

7.        Neymar (Mpira wa miguu): Pauni 85 milioni

8.        Karim Benzema (Mpira wa miguu): Pauni 84 milioi

9.        Stephen Curry (Kikapu): Pauni 80 milioni

10.      Lamar Jackson (Magongo): Pauni 79 milioni.