Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luis Enrique ashtukia janja ya Arsenal

PSG Pict

Muktasari:

  • PSG imeweka rekodi ya kutopoteza mechi ugenini kwa muda mrefu zaidi katika ligi tano bora barani Ulaya na sasa inalenga kuendeleza rekodi hiyo kwa kutopoteza mechi yoyote ya Ligue 1 msimu huu inapokutana na Nice leo, Aprili 25 na itakuwa timu ya kwanza katika historia ya Ligue 1 kumaliza msimu mzima bila kupoteza.

PARIS, UFARANSA: KOCHA wa Paris Saint Germain, Luis Enrique anaamini Arsenal itatumia mbinu za kupaki basi kama itatangulia kufunga bao la mapema.

Arsenal itaikaribisha PSG nyumbani Emirates katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mbaingwa Ulaya na timu hizo zinawania kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hizo na Kocha Mikel Arteta anafurahia kuwa na muda wa kutosha tangu mchezo wa juzi Jumatano dhidi ya Crystal Palace hadi Aprili 29.

Arsenal iliyokuwa ikutane na Palace Jumamosi, zilicheza juzi ili kupisha mchezo wa nusu fainali kombe la FA wa Palace dhidi ya Aston Villa.

Sasa kuelekea mchezo huo utakaopigwa Aprili 29, Enrique alisema anaiona Arsenal itakavyobadilika ikipata bao mapema kama ilivyofanya kwa Real Madrid na muda mwingi ilikuwa ikikaa nyuma kabla ya kupata mabao ya kushtukiza.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Nantes, Jumanne, Enrique alisema: "Wakifunga bao la mapema huenda wakajilinda kwa kucheza chini zaidi. Mwanzoni, wataanza kwa kushambulia kwa nguvu zaidi. Sisi tutajipanga kulingana na hali hiyo."

PSG imeweka rekodi ya kutopoteza mechi ugenini kwa muda mrefu zaidi katika ligi tano bora barani Ulaya na sasa inalenga kuendeleza rekodi hiyo kwa kutopoteza mechi yoyote ya Ligue 1 msimu huu inapokutana na Nice leo, Aprili 25 na itakuwa timu ya kwanza katika historia ya Ligue 1 kumaliza msimu mzima bila kupoteza.