Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mudryk afaulu mtihani wa uongo

MUDRICK Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, kwa sasa amesimamishwa akingojea matokeo zaidi ya sampuli ya haja ndogo ambayo ilionyesha kuwa na viashiria kuwa ametumia dawa zilizozuiwa.

LONDON, ENGLAND: INAELEZWA staa wa Chelsea, Mykhailo Mudryk amefaulu mtihani wa kifaa cha kubaini kama anasema uongo au laa, ikiwa ni katika juhudi za kukusanya ushahidi na kusafisha jina lake dhidi ya tuhuma za kutumia dawa zilizokatazwa michezoni zinazomkabili.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, kwa sasa amesimamishwa akingojea matokeo zaidi ya sampuli ya haja ndogo ambayo ilionyesha kuwa na viashiria kuwa ametumia dawa zilizozuiwa.

Mudryk alisajiliwa kutoka Shakhtar Donetsk ya Ukraine mwaka 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa klabu yake ya zamani, Sergei Palkin, ndiye aliyethibitisha kwamba mchezaji huyo alifanyiwa mtihani huo wa kugundua kama anasema ukweli au laa ulioandaliwa na mawakili wake.

“Nimezungumza na Mudryk mara nyingi tangu suala hili lilipotokea. Kiukweli hajui chochote. Mawakili wake walimpa mtihani wa kifaa cha kubaini uongo, na alifaulu. Hii itakuwa sehemu ya ushahidi unaoonyesha kwamba hakufanya jambo lolote kwa makusudi.”

“Mudryk amekuwa akisema wazi kwamba si kosa lake kwamba alipanga kutumia dawa haramu. Sasa mawakili wanapambana kugundua jinsi hili lilivyotokea, na nani alifanya hivyo.”

Kutumia dawa ya kuongeza nguvu michezoni bila ya kujua haimuepushii mtu adhabu ingawa inaweza kusaidia kuipunguza hukumu ya kufungiwa miaka minne.