Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Tonali, Manchester United bado lipo hai England

Muktasari:

  • Tonali anaendelea kuwa mmoja kati ya viungo wanaowindwa sana Ulaya na uamuzi wa Newcastle United unaweza kusababisha ushindani mkubwa sokoni kuwania saini yake.

MANCHESTER United imepata nafuu katika harakati za kumsajili kiungo wa Italia, Sandro Tonali 25, kutoka Newcastle United baada ya kuambiwa timu hiyo itakuwa tayari kuuza baadhi ya wachezaji muhimu ikiwa ofa sahihi itawasilishwa mwisho wa msimu huu.

Tonali anaendelea kuwa mmoja kati ya viungo wanaowindwa sana Ulaya na uamuzi wa Newcastle United unaweza kusababisha ushindani mkubwa sokoni kuwania saini yake.

Hata hivyo, ili kumpata Man United itatakiwa kushinda vita dhidi ya vigogo wengine Ulaya ikiwamo majirani zao wa Man City ambao wameanza kumuwania huyo hivi karibuni.

Man United imekuwa ikipambana kumsajili kwa sababu inatafuta mbadala wa Casemiro ambaye ameshatangaza kuwa ataondoka mwisho wa msimu.

Newcastle inaweza kuhitaji zaidi ya Pauni 70 milioni ili kumuuza Tonali.


Elliot Anderson

MANCHESTER City inaonekana kuwa mbele ya Manchester United katika vita ya kuiwania saini ya  kiungo wa Nottingham Forest na England, Elliot Anderson, 23, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inaelezwa Man City inataka kusukuma kwa nguvu dili hilo ili likamilike kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia. Anderson anaonekana kuwa mmoja wa viungo vijana wanaochipukia kwa kasi England, jambo linalofanya uwepo ushindani wa kumpata.


Francisco Conceicao

LIVERPOOL imeonyesha nia ya kumsajili winga wa Ureno, Francisco Conceicao, 23, kutoka Juventus kama mbadala wa Mohamed Salah, 33. Inaelezwa kuwa Liverpool inaamini staa huyo anaweza akavaa viatu vya Salah ambaye anandoka mwisho wa msimu huu. Conceicao anaonekana kuwa chaguo linalofaa kutokana na kasi yake na uwezo mkubwa wa kufunga ambao ameuonyesha hadi sasa. Kuna timu kibao Ulaya zinamtaka.


Joao Gomes

MANCHESTER United ni miongoni mwa timu zinazomuwania kiungo wa Brazil, Joao Gomes, 25, anayekipiga Wolves. Inaelezwa kuwa Gomes anaweza kuuzwa kwa takriban Pauni 39 milioni iwapo Wolves itashuka daraja msimu huu, jambo linaloonekana kuwa na nafasi kubwa ya kutokea kwani yao kwa sasa ni mbaya wanaburuza mkia katika msimamo wa ligi. Anasakwa kwa uwezo wake wa kukaba na nguvu.


Phil Foden

BAYERN Munich haina mpango wa kumsajili kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya  England, Phil Foden, 25, licha ya kudaiwa kuwa ipo katika mazungumzo. Inaelezwa sababu kubwa inayowafanya Bayern kujiondoa ni ukosefu wa bajeti ya kutosha kukamilisha uhamisho huo ambao ungehitaji ada kubwa kutokana na thamani ya Foden sokoni. Kwa sasa Bayern imeelekeza nguvu zake katika machaguo mengine ya usajili.


Hugo Ekitike

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Hugo Ekitike, 23, ameongezwa katika orodha ya wachezaji ambao Real Madrid inataka kuwasajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Staa huyo wa Liverpool hajawa na msimu bora hadi sasa, lakini kiwango chake akiwa na Ufaransa kimeonekana kuivutia Real Madrid ambayo imekuwa ikimfuatilia kwa muda sasa. Haijajulikana ikiwa Liverpool itakuwa tayari kumwachia.


Tino Livramento

ARSENAL na Manchester City zinaonekana kuwa vinara wa mbio za kumsajili beki wa Newcastle United United na timu ya taifa ya England, Tino Livramento, 23, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Hata hivyo, dili hilo huenda likafanyika ikiwa Livramento atashindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya na Newcastle. Mkataba wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.


Joshua Zirkzee

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uholanzi, Joshua Zirkzee, 24, anadaiwa kutaka aendelee kubaki Man United msimu ujao, licha ya kutopata nafasi ya kutosha kikosini. Zirkzee inadaiwa anaamini atapata nafasi zaidi ya kucheza chini ya kocha Michael Carrick iwapo ataendelea kubaki. Tangu atue Carrick a amekuwa akipewa nafasi ya kucheza akitokea benchi jambo ambalo lilikuwa gumu kipindi cha Ruben Amorim.