Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Ederson boksa moja miaka minane

BOKSA Pict

Muktasari:

  • Mbrazili huyo alisema amekuwa akivaa boksa hiyo ya aina moja kwa kipindi cha miaka minane kila kipindi anachoingia uwanjani kwenye mechi.

MANCHESTER, ENGLAND: KIPA namba moja wa Manchester City, Ederson amefichua kuna kitu amekuwa akikifanya kama imani kwake, kuvaa nguo ya ndani moja kwa kipindi cha miaka minane.

Mbrazili huyo alisema amekuwa akivaa boksa hiyo ya aina moja kwa kipindi cha miaka minane kila kipindi anachoingia uwanjani kwenye mechi.

Miaka minane ina maana ni kipindi chote alichokuwa kwenye kikosi cha Etihad baada ya kunaswa na kocha Pep Guardiola akitokea Benfica mwaka 2017.

Ederson alijiunga na Man City kwa dau la Pauni 35 milioni na ilikuwa msimu wa pili wa kocha Guardiola baada ya kushindwa kubeba ubingwa kwenye msimu wake wa kwanza.

Kipa Ederson ameichezea Man City mechi 362 na kunyakua mataji sita ya Ligi Kuu England, Kombe la FA mara mbili, Kombe la Ligi mara nne, Ligi ya Mabingwa Ulaya mara moja, sawa na UEFA Super Cup na Kombe la Dunia la Klabu ndani ya muda huo.

Kipa Ederson alisema: “Nimekuwa na kitu kimoja nimekuwa nikikifanya kama imani. Kucheza kila mechi na boksi ileile.”

Hilo alizungumza na kipa Shay Given, aliyemuuliza: “Nini, boksi moja msimu mzima?”

“Hapana, miaka minane boksa moja,” alifafanua Ederson huku akionyesha tabasamu, jambo ambalo lilimshangaza Given, na kusema: “Haiwezekani,” na kusema “Lazima itakuwa haipo kwenye mwonekano mzuri!”