Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FIFA yaja na kanuni mpya Kombe la Dunia 2026

FIFA Pict

Muktasari:

  • Mchakato huu pia utatumika kwenye ligi mbalimbali msimu wa 2026-27, huku FIFA ikitumia mfano wa michuano ya National Women’s Soccer League ya Marekani.

ZURICH, USWISS: SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA), limeamua kuzuia wachezaji kwenda kwenye eneo la kiufundi kuzungumza na makocha wao wakati mlinda mlango akitibiwa majeraha katika michuano ya Kombe la Dunia 2026, kwa mujibu wa Pierluigi Collina, mmoja wa mabosi wa shirikisho hilo.

Hatua hii inatokea baada ya kuibuka kwa mbinu ya makipa kudanganya kuwa wameumia ili wachezaji wenzake wapate nafasi ya kwenda kuzungumza na makocha kwenye benchi la ufundi.

Kwa mujibu wa IFAB, wachezaji wote wanapaswa kubaki pale walipo au kukaa katikati ya uwanja endapo kipa atakuwa ameumia na madaktari kuingia kumtibu badala ya kwenda pembeni mwa uwanja kupewa ushauri wa makocha.

Collina amesema: “Mlinda mlango ana haki ya kujeruhiwa, lakini wachezaji hawana haki ya kuondoka uwanjani kwa mazungumzo na kocha hii ni sheria mpya na kila timu itakuwa inafahamu hilo.”

Kuna mambo mengi mapya yataonekana kwenye kanuni mpya za Kombe la Dunia msimu huu, hii ni mojawapo kwa kuwa makocha wamekuwa wakiitumia sana,” amesema bosi huyo.

Mbali na hiyo kuna kanuni mpya ya wachezaji kupigwa marufuku kusukumana, kushikana, kuvutana na mmoja kumzuia mwenzake asipite mbele wakati ambapo kona inapigwa. Mfumo wa kuwazuia wapinzani umetumiwa zaidi na Arsenal kwenye Ligi Kuu England msimu huu hali iliyowafanya wafanikiwe kutwaa ubingwa.

Mchakato huu pia utatumika kwenye ligi mbalimbali msimu wa 2026-27, huku FIFA ikitumia mfano wa michuano ya National Women’s Soccer League ya Marekani.