Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Iraq; Simba wanaorudi kombe la dunia 2026

IRAQ Pict

Muktasari:

  • Timu yao ya taifa inayojulikana kama ‘Lions of Mesopotamia’ lenye maana ya Simba wa Mesopotamia, jina linalotokana na historia ya ustaarabu katika miaka hiyo uliokuwa katika eneo la mito ya Tigris na Euphrates ndani ya Iraq.

BAGHDAD, IRAQ: IRAQ ambako anacheza soka la kulipwa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ni moja ya mataifa yenye historia kubwa ya soka huko Mashariki ya Kati na bara la Asia.

Timu yao ya taifa inayojulikana kama ‘Lions of Mesopotamia’ lenye maana ya Simba wa Mesopotamia, jina linalotokana na historia ya ustaarabu katika miaka hiyo uliokuwa katika eneo la mito ya Tigris na Euphrates ndani ya Iraq.

Mesopotamia ilikuwa moja ya maeneo ya mwanzo kabisa duniani kuwa na ubinadamu, hivyo jina hilo linaashiria nguvu, urithi wa kihistoria na moyo wa mapambano unaoibeba timu ya taifa ya Iraq.

Timu hiyo imekuwa alama ya matumaini, uzalendo na umoja kwa wananchi wa Iraq kwa miaka mingi hata katika vipindi vigumu vya vita na changamoto za kisiasa. Wababe hao kutoka Asia hii itakuwa mara yao ya pili kucheza Fainali za Kombe la Dunia huku wakiwa na kibarua kizito katika kundi I dhidi ya Senegal, Ufaransa na Norway.

IRA 01


WAPI WALIANZIA

Oktoba 8, 1948, Shirikisho la Soka Iraq lilianzishwa huku likijiunga na FIFA 1950 na Aprili 1951 Iraq ilicheza mechi yake ya kwanza ambapo iliifunga timu ya Civil Cantonment (CC) ya Habbaniyah kwa mabao 5–0. Mechi ya kwanza rasmi ya kimataifa ya Iraq ilifanyika katika mchezo wa ufunguzi wa Michezo ya Kiarabu ya mwaka 1957 ahuko Beirut ambapo Iraq ilitoka sare ya mabao 3–3 dhidi ya Morocco.

Mabao ya Iraq yalifungwa na Ammo Baba, Youra Eshaya (wote kutoka jamii ya Waashuri wa Iraq) pamoja na Fakhri Mohammed Salman. Mmoja wa wachezaji wa timu ya kwanza ya taifa ya Iraq alikuwa Youra Eshaya, ambaye mwaka 1954 alikua mchezaji wa kwanza wa Iraq kucheza nchini Uingereza akiwa katika klabu ya Bristol Rovers Colts.

Iraq ilitwaa kombe lake la kwanza mwaka 1964 baada ya kushinda Kombe la Kiarabu ambapo ilishinda michezo mitatu na kutoka sare moja kati ya michezo minne. Katika mashindano yaliyofuata, Iraq ilitetea ubingwa wake wa Kombe la Kiarabu kwa kuifunga Syria mabao 2–1 kwenye fainali iliyochezwa Baghdad.

IRA 02

MAPIGO NA MWENDO

Mwaka 1972, Iraq ilishiriki kwa mara ya kwanza katika Kombe la Mataifa ya Asia (AFC Asian Cup) lakini haikushinda mchezo wowote kwenye mashindano hayo. Machi 1973, Iraq ilianza kampeni yake ya kwanza ya kufuzu Kombe la Dunia la FIFA.

Walimaliza nafasi ya pili katika kundi lao, pointi moja nyuma ya Australia, hivyo wakashindwa kufuzu hatua iliyofuata. Katika miaka iliyobaki ya 1970, Iraq ilifika hatua ya pili ya Michezo ya Asia mwaka 1974, ilipoteza fainali ya Kombe la Ghuba ya Kiarabu mwaka 1976, ilimaliza nafasi ya nne katika AFC Asian Cup mwaka 1976, ilimaliza nafasi ya nne katika Michezo ya Asia mwaka 1978 na hatimaye ikaandaa na kushinda Kombe la Ghuba ya Kiarabu mwaka 1979. Kombe la Asia la mwaka 1976 lilikuwa la mwisho kwa Iraq kushiriki kwa kipindi cha miaka 20 iliyofuata, kwani walijiondoa katika mashindano matatu yaliyofuata ya mashindano hayo.


KOMBE LA DUNIA 1986

Katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi B kwenye Kombe la Dunia 1986, Iraq ilicheza vizuri dhidi ya Paraguay lakini ikapoteza kwa mabao 1–0, licha ya kufunga bao ambalo lilikataliwa kwa utata na mwamuzi. Katika mchezo wa pili, Iraq ilifunga bao lake la kwanza kabisa katika historia ya Kombe la Dunia kupitia Ahmed Radhi dhidi ya Ubelgiji, lakini walipoteza kwa mabao 2–1 licha ya kucheza wakiwa pungufu kwa mchezaji mmoja. Katika mchezo wa tatu, Iraq ilicheza dhidi ya wenyeji Mexico na kupoteza kwa bao 1–0.

IRA 03

KIPINDI CHA GIZA

Baada ya vita vya Ghuba 1990, Iraq ilipigwa marufuku kushiriki michezo ya Asia na mashindano mengi ya Kiarabu.

Hata hivyo, marufuku hiyo haikuhusisha Kombe la Dunia. Mwaka 1993, Iraq ilishiriki katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia 1994. Katika hatua ya kwanza, Iraq ilikuwa kundi moja na China, Yemen, Jordan na Pakistan.

Katika hatua ya mwisho ya kufuzu, Iraq ilikuwa kundi moja na Saudi Arabia, Korea Kusini, Japan, Iran na Korea Kaskazini. Katika mchezo wa kwanza, Iraq ilipoteza kwa mabao 3–2 dhidi ya Korea Kaskazini katika mchezo wa kusisimua baada ya kuwa inaongoza kwa mabao 2–0 kipindi cha pili. Baada ya mchezaji wa Iraq kutolewa nje kwa kadi nyekundu, Korea Kaskazini ilichomoa bao la kwanza katika dakika ya 67, ikasawazisha dakika ya 77 na kufunga bao la ushindi dakika ya 82.

Iraq baadaye ilitoka sare ya 2–2 dhidi ya Korea Kusini, kisha ikaifunga Iran mabao 2–1, ilikosa nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia kwa tofauti ya pointi mbili. Kwa kutoka sare ya mabao 2–2 dhidi ya Japan katika mchezo wao wa mwisho, Iraq iliinyima Japan nafasi ya kufuzu kwenye fainali za Kombe la Dunia. Kipigo dhidi ya Korea Kaskazini ndicho kilichoathiri zaidi nafasi ya Iraq, kwani Korea Kaskazini ilipoteza michezo yake mingine minne na kumaliza mkiani mwa kundi.


SIMBA WALIVYOJIPATA 

Novemba 7, 2022, Jesus Casas aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Iraq, akiwa na mkataba wa miaka minne (2026). Katika mashindano yake ya kwanza akiwa kocha, Iraq ilikuwa mwenyeji wa Kombe la 25 la Ghuba ya Kiarabu (Arabian Gulf Cup) na ikashinda taji hilo baada ya kuifunga Oman mabao 3–2. Katika hatua ya pili ya kufuzu Kombe la Dunia, Iraq iliwekwa katika Kundi F pamoja na Vietnam, Ufilipino na Indonesia. Timu ilifanya vizuri, ikishinda michezo yote sita, hivyo ikafuzu kwenda hatua inayofuata pamoja na kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Asia.

IRA 04

MASTAA WAO

Aymen Hussein ni mmoja wa washambuliaji muhimu zaidi wa kizazi cha sasa cha Iraq, amefunga mabao tisa na kutoa asisti moja katika michezo 16 ya Ligi Kuu nchini humo.

Kabla ya kurejea zake Iraq, Hussein alikuwa akicheza Qatar akiwa na klabu ya Al-Khor SC. 

Nyota mwingine wa Iraq ni Amir Al-Ammari ambaye ni kiungo wa kati anayejulikana kwa uwezo wake wa kutuliza na kuongoza mchezo. Ana mchango mkubwa katika kupangilia mashambulizi na pia kusaidia kulinda huyu ndiye mtaalamu wa mipira ya penalti na mipira ya adhabu.