Black Stars tayari kwa Kombe la Dunia 2026
Muktasari:
- Kocha mkuu wa Black Stars, Carlos Quiros, tayari ameshatangaza kikosi kitakachoingia kambini, kabla ya kuanza safari ya kuelekea Marekani kwa fainali hizo ambazo zitafanyika pia Mexico na Canada.
Chama cha Soka cha Ghana (GFA), kimeachia video maalum inayoonyesha kambi ya timu ya taifa hilo maarufu Black Stars, iliyoko Cardiff, Wales tayari kwa maandalizi ya Fainali za Kombe la Dunia 2026.
Kocha mkuu wa Black Stars, Carlos Quiros, tayari ameshatangaza kikosi kitakachoingia kambini, kabla ya kuanza safari ya kuelekea Marekani kwa fainali hizo ambazo zitafanyika pia Mexico na Canada.
Video iliyoachiwa na GFA inaonyesha sehemu mbalimbali za kambi hiyo ambazo zitawahusisha maafisa wa benchi la ufundi na wachezaji.
Kikosi kilichotajwa na kocha Carlos Quiros kipo hivi; Makipa: Benjamin Asare, Lawrence Ati-Zigi, Joseph Anang, Solomon Agbasi na Paul Reverson.
Mabeki: Baba Abdul Rahman, Gideon Mensah, Marvin Senaya, Alidu Seidu, Abdul Mumin, Jerome Opoku, Jonas Adjetey, Kojo Oppong Peprah na Alexander Djiku.
Viungo: Elisha Owusu, Thomas Partey, Kwasi Sibo, Augustine Boakye, Caleb Yirenkyi na Abdul Fatawu Issahaku.
Washambulaiji: Kamal Deen Sulemana, Christopher Bonsu Baah, Ernest Nuamah, Antoine Semenyo, Brandon Thomas-Asante, Prince Kwabena Adu, Inaki Williams na Jordan Ayew.