Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gary Neville: Man City v United wachezaji hawakucheza kama Dabi

Muktasari:

  • Chama hicho cha soka kinataka kubadilisha mambo katika kikosi cha mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia na kurudisha hadhi ya timu hiyo ya taifa linalotambulika kwa kutoa vipaji vikubwa vya soka.

ISTANBUL, UTURUKI: TOVUTI ya Globo imefichua kocha wa Fenerbahce, Jose Mourinho yupo katika orodha ya makocha ambao chama cha soka cha Brazil kinataka kuwaajiri.

Chama hicho cha soka kinataka kubadilisha mambo katika kikosi cha mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia na kurudisha hadhi ya timu hiyo ya taifa linalotambulika kwa kutoa vipaji vikubwa vya soka.

Brazil imeshinda mataji matano katika miaka ya 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002 na kutoa vipaji vingi vilivyotamba duniani na kuitangaza vema nchi hiyo.

Mourinho ni kati ya makocha waliotajwa huenda wakapewa timu hiyo, licha ya awali mwenyewe kudai hapendelei sana kufundisha timu za taifa na atajikita zaidi katika klabu.

Makocha wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni pamoja na Carlo Ancelotti anayepewa nafasi kubwa, Jorge Jesus na Abel Ferreira.

Ancelotti anapewa nafasi kubwa kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonyesha akiwa na kikosi cah Real Madrid na Brazil inaona kama ndiye kocha mwafaka wa kurudisha makali ya kikosi hicho ambacho mara ya mwisho kubeba Kombe la Dunia ilikuwa ni mwaka 2002.

Kwa upande wa Mourinho, kinachombeba kupata kazi katika kikosi hicho ni lugha kwani anazungumza Kireno kwa ufasaha, pia inatajwa uzoefu wake wa kutosha katika kufundisha soka na mafanikio aliyoyapata akiwa na wachezaji kadhaa wa taifa hilo ni sababu ya  kuwekwa kwenye orodha hiyo.

Mourinho mwenye umri wa miaka 62, amezifundisha timu nyingi kubwa Ulaya zikiwamo, FC Porto, Inter Milan, Chelsea, Real Madrid, Manchester United na Tottenham akitwaa pia mataji makubwa likiwamo maarufu zaidi la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Amebeba pia vikombe vya ligi za ndani za England, Hispania na Ureno na kuwa mmoja wa makocha wakubwa walioshinda kila taji Ulaya katika timu alizopita.

Ni wazi taji ambalo hana kocha huyo anayejulikana pia kama ‘The Special One’ ni linaloshirikisha timu za taifa likiwamo Kombe la Dunia na atalisaka taji hilo endapo atapata kazi hiyo.