Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maamuzi magumu Man United, Amorim kuhusika

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Licha ya kusajili, pia kuna orodha ya wachezaji ambao Mashetani Wekundu wanatarajia kuachana nao ili kupata pesa za kusajili pia kutokana na viwango vyao kutoridhisha.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United itaingia kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi ikiwa na mpango wa kutaka kuboresha kikosi chake huku kocha mpya Ruben Amorim akitarajiwa kupata fursa yake ya kwanza ya kuunda kikosi akitakacho baada ya miezi kadhaa ya kutathmini wachezaji aliowakuta kikosini katika msimu huu mgumu kwao.

Licha ya kusajili, pia kuna orodha ya wachezaji ambao Mashetani Wekundu wanatarajia kuachana nao ili kupata pesa za kusajili pia kutokana na viwango vyao kutoridhisha.

Hadi sasa tayari zimeibuka ripoti kwamba Andre Onana anaweza kutimkia Saudi Arabia kwa sababu kocha haridhishwi na kiwango chake ingawa yeye mwenyewe bado anahitaji kuendelea kusalia katika kikosi hicho.

Mbali ya Onana, kipa namba mbili Altay Bayindir, naye anaonekana katika hatari kubwa ya aidha kutolewa kwa mkopo au kuuzwa jumla katika dirisha lijalo kwa sababu kiwango chake hakionekani kumpa changamoto Onana.

Beki wa kati, Harry Maguire ambaye katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi alihusishwa na timu nyingi lakini ilishindikana kuuzwa, Man United inataka kumtumia kama sehemu ya ofa ya kumpata beki kisiki wa Everton, Jarrad Branthwaite.

Mchezaji mwingine ni Luke Shawambaye amekuwa akisumbuliwa naye anaonekana kuwa katika mstari mwekundu wa kuuzwa na hiyo imezidi baada ya kusajiliwa kwa Patrick Dorgu Januari, mwaka huu.

Mchezaji mwingine anayeonekana kuwa katika hatari ni Mason Mount, ambaye naye amekuwa na majeraha ya mara kwa mara.

Katika eneo la ushambuliaji mastaa kama  Ramus Hojlund na Joshua Zirkzee nao wanaonekana kuwa na nafasi ndogo za kubakia kutokana na viwango vyao na huenda Amorim akahitaji washambuliaji wapya watakaompa mabao zaidi.

Kobbie Mainoo alikuwa akihusishwa kuondoka tangu Januari mwaka huu baada ya kugoma kusaini mkataba mpya ambapo vigogo wa Man United waliona wamuuze mapema wakati mkataba wake wa sasa ukielekea kumalizika mwaka 2027.

Alejandro Garnacho ambaye alikuwa katika kapu moja na Marcus Rashford ingawa yeye ameendelea kubadilika, naye hayupo salama na tayari timu kama Atletico Madrid zimeanza kuinyatia huduma yake.