Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jurgen Klopp anarudi uwanjani

KLOPA Pict

Muktasari:

  • Klopp ambaye kwa sasa anahudumu kama mkuu wa upande wa soka kwa timu zinazomilikiwa na kampuni ya Red Bull, aliondoka Liverpool baada ya kuhudumu kwa miaka tisa na kushinda mataji makubwa ya ndani na nje ya England.

MADRID, HISPANIA: KOCHA wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp inadaiwa anafikiria kurejea katika kazi yake hiyo ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu alipoondoka Anfield mwishoni mwa msimu wa 2023/24.

Klopp ambaye kwa sasa anahudumu kama mkuu wa upande wa soka kwa timu zinazomilikiwa na kampuni ya Red Bull, aliondoka Liverpool baada ya kuhudumu kwa miaka tisa na kushinda mataji makubwa ya ndani na nje ya England.

Mara kadhaa amekuwa akihitajika na timu mbalimbali barani Ulaya lakini amekuwa akikataa na kusisitiza bado anahitaji kupumzika.

Hata hivyo, timu hizo zimezidi kutaka kumsajili na kwa mujibu wa tovuti ya TBR Football, kwa sasa kuna timu tatu zinazomhitaji kuelekea msimu ujao.

Timu ya kwanza ni Real Madrid ambayo inamwangalia Mjerumani huyu kama mbadala wa Kocha wao Carlo Ancelotti ambaye anahusishwa anaweza akaondoka mwisho wa msimu kujiunga na timu ya taifa ya Brazil.

Muitaliano huyo ambaye ameshinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa akiwa na Madrid, amekuwa akipewa nafasi ya kuwa kocha wa Brazil kwa muda sasa na uvumi umeongezeka baada ya taifa hilo kumfukuza Dorival kutokana na kipigo cha 4-1 walichopata kutoka kwa Argentina.

Mbali ya Klopp, Madrid pia inamwangalia Kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso.

Timu ya taifa ya Marekani pia bado inamwangalia Klopp licha ya sasa kuwa na Mauricio Pochettino ambaye ilimwajiri baada ya kumkosa Klopp kwa wakati huo.

Inaelezwa, mabosi wa chama cha soka cha Marekani wanaweza kufanya maamuzi magumu ya kumfukuza Pochettino kwa sababu hawaridhishwi na maendeleo ya timu na bado wanamfikiri Klopp kama mtu sahihi.