Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matano muhimu gemu 3 NBA

Muktasari:

  • Ikiwa mechi mbili za mwanzo zilijkuwa na ushindani mkubwa na tofauti ya jumla ya alama tano, mchezo wa tatu maarufu kama ‘Game 3’ uliochezwa katika ukumbi mpya wa kifahari wa Intuit Dome jijini Los Angeles ilikuwa kama filamu ya aina nyingine.

 LOS ANGELS MAREKANI : KATIKA mchezo wa tatu wa mchuano wa kwanza wa hatua ya mtoano wa NBA kati ya Los Angeles Clippers na Denver Nuggets, hali imebadilika.

Ikiwa mechi mbili za mwanzo zilijkuwa na ushindani mkubwa na tofauti ya jumla ya alama tano, mchezo wa tatu maarufu kama ‘Game 3’ uliochezwa katika ukumbi mpya wa kifahari wa Intuit Dome jijini Los Angeles ilikuwa kama filamu ya aina nyingine.

Clippers waliibuka na ushindi wa pointi 117-83, ushindi wa tofauti wa alama 34 uliowalazimisha Nuggets kujitathimini upya.

Huo ni ushindi wa pili kwa Clippers katika mfululizo wa mechi tano na sasa wanaongoza mfululizo huo kwa 2-1.

Haya hapa ni mambo matano muhimu muhimu kutoka ‘Game 3’:


1. Nikola JokiC Amechoka?

Nikola Jokic, mshindi wa tuzo ya MVP mara tatu alionekana kuwa na wakati mgumu uwanjani. Ingawa alimaliza na tarakimu mbili (10 au zaidi) katika vipengele vitatu tofauti vya takwimu kuu za mchezo katika mechi moja ‘triple-double’  ya 23-13-13, haikuleta maana yoyote kutokana na kipigo kikubwa walichopokea. Nyota huyo alionekana kuchoka kimwili na kiakili hasa baada ya kutumia dakika 46 kwenye ‘Game 1’ yaani mchezo wa kwanza akicheza kila dakika kipindi cha pili cha ‘Game 2’ (mchezo wa pili).

Pamoja na juhudi zake binafsi, wachezaji wenzake hawakufua dafu na hawajaonyesha kiwango kinachokaribiana naye. Jokic alionekana akipandisha sauti na kuonyesha hasira kwenye muda wa mapumziko kipindi cha pili ishara ya kuchoshwa na hali ya kubeba mzigo peke yake.


2. Ivica Zubac anamsumbua JokiC

Kwa nadra, Jokic hakuonekana kuwa mchezaji bora wa nafasi ya kati uwanjani. Ivica Zubac wa Clippers alicheza kwa kiwango cha juu akifunga pointi 20 kwa ufanisi mkubwa na kulazimisha Nuggets kumuwekea ulinzi wa watu wawili katika baadhi ya vipindi.

Zubac ambaye ni mmoja wa wachezaji wanaowania tuzo ya Mchezaji Aliyeimarika Zaidi (Most Improved Player), ameonyesha maendeleo makubwa si tu katika ulinzi, bali pia katika kushambulia. Tofauti ya pointi na ‘rebound’ kati yake na Jokic‡ ilikuwa ndogo, lakini tofauti ya mchango kwa timu ilikuwa kubwa kwa faida ya Clippers.


3. Clippers WakoMoto

Los Angeles Clippers wamepata ushindi katika michezo 20 kati ya 24 iliyopita wakiwa na takwimu za kutisha. Ushindi wa Game 3 haukuwa bahati mbaya kwao, bali ni mwendelezo wa fomu nzuri waliyoingia nayo baada ya kujinasua kwenye kundi la ‘play-in’. Kwa msaada wa nyota wawili, Kawhi Leonard na James Harden pamoja na wachezaji wa akiba kama Norman Powell na Kris Dunn aliyeimarika upande wa ulinzi, Clippers wanaonekana kuwa tishio.

Kocha Tyronn Lue ameonyesha kuwa na uelewa mkubwa wa mbinu na namna ya kuwapa wachezaji wake nguvu mpya kila mchezo. Clippers sio tu ni timu bora zaidi kwa uwezo, lakini wanaonekana kuwa timu ya hatari zaidi kwa sasa.


4. Kisa na Mkasa wa Russ

Russell Westbrook (Russ), aliyewahi kuwa mchezaji wa Clippers kwa misimu miwili iliyopita hakupata ndoto ya kulipiza kisasi mbele ya waajiri wake wa zamani. Alipata majeraha ya mguu wa kushoto wakati wa mazoezi ya kabla ya mchezo, na alicheza dakika tisa tu kabla ya kuondoka uwanjani kutokana na kuvimba kwa mguu.

Kwa Denver Nuggets, hilo ni pigo hasa ukizingatia kuwa benchi la wazhezaji limekuwa na changamoto kubwa msimu huu. Upungufu wa nguvu kutoka kwa wachezaji wa akiba pamoja na hali ya kutotabirika ya Westbrook, ni sababu nyingine inayochochea matatizo ya Nuggets.


5. Intuit Dome Yatoa Nguvu Mpya

Game 3 ilikuwa mechi ya kwanza ya mtoano kwa Clippers katika uwanja wao mpya wa Intuit Dome, na mazingira yalionekana kutoa nguvu kwa wenyeji. Uwanja huo wa thamani ya mabilioni ya dola ulitawaliwa na shamrashamra, na sehemu ya nyuma ya eneo la wageni maarufu kama The Wall ilikuwa kama ngome ya mashabiki waliokuwa na furaha.