Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maresca: Sijakimbia mashabiki

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Blues aliwapa mkono wasaidizi wake wa benchi la ufundi kisha akaelekea moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akiwaacha wachezaji wakisherehekea ushindi.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amesisitiza kuondoka kwake haraka mara tu filimbi ya mwisho ilipopigwa katika mchezo dhidi ya Fulham wikiendi iliyopita, ilikuwa ni kwa sababu ya kuwaachia wachezaji wa Chelsea wafurahie ushindi wa kusisimua na sio kukataa kukutana na mashabiki ambao walikuwa wakiimba kwamba afukuzwe.

Kocha huyo wa Blues aliwapa mkono wasaidizi wake wa benchi la ufundi kisha akaelekea moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akiwaacha wachezaji wakisherehekea ushindi.

Maresca pia amesisitiza hadi sasa anaona timu yake ina mafanikio makubwa kwani katika miaka mitatu iliyopita hawaikuwahi kuwa kwenye nafasi iliyopo Ligi Kuu England.

Kocha huyu alisema bao la Pedro Neto lililowahakikishia ushindi halijabadilisha msimu kwa namna yoyote.

“Bao la Pedro halibadilishi msimu. Tayari nimesema katika miaka mitatu iliyopita hatujawahi kuwa kwenye nafasi za Ligi ya Mabingwa. Hivyo, bao hilo halibadilishi chochote. Tayari huu tumeshafanya vizuri kwa kuwa nafasi tuliyopo sasa,” alisema.

Kocha wa Fulham naye alisema timu bado hawajakata tamaa kwani nafasi ya  kufuzu Europa League au Conference League bado ipo.

“Kila wiki tunacheza kama fainali, kwa hiyo huu ulikuwa ni mchezo muhimu tulioupoteza,” alisema Silva.

“Lakini tunapaswa kuwa na mtazamo wa uwiano katika tathmini yetu kwa sababu kulikuwa na mambo mengi mazuri pia. Huu sio mwisho, bado kuna mengi ya kupigania.”