Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Man United wachoka maneno

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Gwiji huyo wa Old Trafford, Scholes ametengeneza utamaduni wa kuwa mkosoaji mkubwa dhidi ya wachezaji wa klabu yake ya zamani wa Man United kwa miaka ya hivi karibuni ambapo mambo yamekuwa yakienda mrama.

MANCHESTER, ENGLAND: MAMBO ni moto. Mastaa wa Manchester United wameripotiwa kumwita kwenye uwanja wa mazoezi kiungo wa zamani wa miamba hiyo Paul Scholes baada ya kuchoshwa na ukosoaji wake usiokoma.

Gwiji huyo wa Old Trafford, Scholes ametengeneza utamaduni wa kuwa mkosoaji mkubwa dhidi ya wachezaji wa klabu yake ya zamani wa Man United kwa miaka ya hivi karibuni ambapo mambo yamekuwa yakienda mrama.

Scholes, aliyekuwa akimudu nafasi ya kiungo na sasa akiwa amestaafu amekuwa kama kiungo mwingine za zamani wa timu hiyo ya Old Trafford, Roy Keane kutokana na ukosoaji wa muda mrefu wa wachezaji wa timu hiyo pindi mambo yanapokwenda kombo uwanjani. Na Scholes kwenye ukosoaji wake amekuwa akiwalenga aina fulani ya wachezaji, akiwakosoa kila wakati kama vile Bruno Fernandes, Marcus Rashford, Diogo Dalot na wengine.

Kwa mujibu wa Scholes mwenyewe, ambaye ni mshindi mara 11 wa Ligi Kuu England, alisema wachezaji hao hawapendezwi kabisa na maneno yake. Na mmoja wa wachezaji hao walimpigia simu gwiji huyo na kumshambulia.

"Wachezaji wa siku hizi wamekosa uvumilivu," alisema Scholes na kuongeza. "Kuna mchezaji, yupo kwenye timu kwa sasa, mwaka huu aliwasiliana na mimi na kunieleza hafurahishwi na vitu ninavyosema.

"Alitaka tukutane kwenye uwanja wa mazoezi, nilimjibu, 'bila shaka, hakuna tatizo' nilimtajia mawasiliano yangu, hakunitafuta tena. Ningeenda tufanye mazoezi. Kama nasema vitu ninavyoviamini na anataka nielezee kwanini, hayakuwa mazungumzo mazuri, lakini nilimwambia kama kuna mwingine yeyote mwenye shida, namba yangu ni hiyo."

Scholes alikosoa baada ya mechi ya sare ya bila kufungana dhidi ya Manchester City kwenye Manchester derby uwanjani Old Trafford, Jumapili iliyopita. Mastaa wa Man United chini ya kocha Ruben Amorim walikosolewa kwa kushindwa kutumia fursa ya kushuka kiwango kwa mahasimu wao hao ili kuwaadhibu, ambapo mchezaji mwenzake Scholes, Gary Neville, alidai kwamba wachezaji wa Man United walikuwa ni kama maroboti wanaocheza kwa maelekezo.

Beki huyo wa pembeni wa zamani, Neville aliwataka wachezaji wa Man United kupambana kwa jasho la damu kwenye mechi hiyo ili kuhakikisha wanashinda, akidai upambanaji siku hizi haupo na ndio maana timu inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Man United imekuwa kwenye kiwango cha kawaida sana kwa miaka ya karibuni tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson licha ya timu hiyo kupita makocha mahiri kama Erik ten Hag, Jose Mourinho, Louis van Gaal, David Moyes na wengineo.