Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiulaini Arsenal kwa Madrid basi tu UCL

Muktasari:

  • Hata hivyo, kuelekea mechi hiyo Arsenal ni kama washindwe wenyewe tu kwani wanakutana na vigogo hao wa Hispania wakiwa na matatizo mengi kuanzia ndani na nje ya uwanja.

MADRID, HISPANIA: LIGI ya Mabingwa Ulaya inaendelea leo kwa michezo miwili ya robo fainali kupigwa, lakini mechi inayotarajiwa kutazamwa zaidi na watu wengi ni ile kati ya Arsenal na Real Madrid ambayo ni ya mkondo wa pili baada ya ile ya kwanza kumalizika kwa Arsenal kushinda mabao 3-0.

Hata hivyo, kuelekea mechi hiyo Arsenal ni kama washindwe wenyewe tu kwani wanakutana na vigogo hao wa Hispania wakiwa na matatizo mengi kuanzia ndani na nje ya uwanja.

Real Madrid walifanikiwa kupoza machungu ya kichapo cha Arsenal Jumapili iliyopita baada ya kuichapa Alaves kwa bao 1-0 licha ya supastaa Kylian Mbape kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya Antonio Blanco.

Hata hivyo, taarifa zinadai wachezaji wa Real Madrid waligombana siku moja kabla ya mechi hiyo kuchezwa ambapo Jude Bellingham na Antonio Rudiger walipaswa kutenganishwa baada ya kutofautiana katika mazoezi Ijumaa.

Tovuti ya El Chiringuito imeripoti kuwa nyota wa zamani wa Chelsea, Rudiger, alimchezea Bellingham rafu wakati wanafanya mazoezi jambo lililosababisha mchezaji huyo wa kimataifa wa England kumtolea maneno machafu ambayo yalimkasirisha Rudiger kiasi cha kutaka kuzichapa kabla ya wachezaji wenzao kuingilia kati na kuwatenganisha.

Licha ya mvutano huo, inasemekana Bellingham na Rudiger walimaliza tofauti haraka.

Zaidi ya hayo, Real Madrid imepata pigo jingine baada ya kuthibitishwa kuwa beki Ferland Mendy hatacheza mchezo huo. Beki huyo wa kushoto alipata jeraha la msuli wa paja kabla ya mchezo wa kwanza, na sasa gazeti la AS limeripoti kuwa hakuna uwezekano wa kurejea leo.

Hilo linaongeza idadi ya wachezaji watakaokosekana kutokana na majeraha  ikiwa ni pamoja na Eduardo Camavinga aliyepewa kadi nyekundu mwishoni mwa mchezo wa kwanza.

Pia kuna shaka ya majeraha kwa Federico Valverde na David Alaba, huku Dani Ceballos akiwa na hatihati ya kucheza. Habari njema pekee kwa Real ni kurejea kwa Aurelien Tchouameni kutoka kwenye adhabu ya kusimamishwa.

Akizungumzia pambano hilo, Ancelotti alikumbushia nyakati ambapo timu zimewahi kugeuza matokeo makubwa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya akitaja neno “remontada” ambalo lilizaliwa baada ya Barcelona kugeuza kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Paris Saint-Germain 2017 akisema; Akasema: “Remontada? Tutajaribu. Imetokea mara nyingi. Tutajaribu hadi dakika ya mwisho.”

Mchezo mwingine utakaopigwa leo ni kati ya Inter Milan na Bayern Munich ambao utapigwa katika Jiji la Milan kuanzia saa 4:00 usiku.