Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa wenye uhusiano wa karibu na wanyama

Wanyama Pict
Wanyama Pict

Muktasari:

  • Kwa upande wa wachezaji wa soka, licha ya ratiba zao ngumu, baadhi yao wameonyesha mapenzi ya dhati kwa wanyama wao wa kufugwa.

LONDON, ENGLAND: WANYAMA wanapendwa na watu wengi duniani wakichukuliwa kama sehemu ya familia katika nyumba nyingi.

Kwa upande wa wachezaji wa soka, licha ya ratiba zao ngumu, baadhi yao wameonyesha mapenzi ya dhati kwa wanyama wao wa kufugwa.

Kutoka kwa Arsenal, Chelsea, Liverpool hadi Manchester United, wachezaji hawa wana uhusiano wa karibu sana na wanyama wao, wanaouonyesha upande wao wa huruma na ubinadamu. 

Kwa kuwa na fedha nyingi na muda wa kutosha, haishangazi kuona wanasoka wa daraja la juu wakiwaekeza mapenzi na rasilimali nyingi kwa ajili ya ustawi wa wanyama wanaowapenda.

Hawa ni baadhi tu ya wachezaji ambao wamejenga uhusiano wa kipekee na wanyama, kuanzia kwa wapenda mbwa wa kawaida hadi wale wanaohusudu wanyama wa ajabu kama punda na hata simba.


WNY02
WNY02

KAI HAVERTZ

“Baadhi ya wachezaji wenzangu huniita Punda,” alisema Kai Havertz ambaye anaichezea Arsenal na timu ya taifa la Ujerumani, alipokuwa akihojiwa na chombo kimoja cha habari huko England.

“Tangu mwanzo, nilihisi uhusiano wa karibu na punda. Ni wanyama watulivu sana; pengine ninajifananisha nao kwa sababu mimi pia ni mtulivu. Wanapumzika siku nzima, hawafanyi mengi, wanataka tu kuishi maisha yao. Nimewapenda daima.” 

Havertz alieleza jinsi alivyotembelea hifadhi ya punda kama sehemu ya kupumzika kiakili baada ya matokeo mabaya uwanjani. Alipata utulivu na amani kwa kuwatazama wanyama hao, akiona kitu cha kibinadamu ndani yao. 

Uhusiano huu wa pekee ulimfanya kuanzisha shirika la misaada, Kai Havertz Stiftung, lenye lengo la kusaidia ustawi wa wanyama, kuendeleza vijana, na kuwasaidia wazee. 


MARIO BALOTELLI

Mshambuliaji wa Genoa, Balotelli haishangazi kwamba ana mahusiano wa karibu na wanyama wa kila aina. Mbali na mbwa, Balotelli pia anapenda nguruwe.

“Mwishowe nguruwe wangu mdogo amewasili!” aliandika Balotelli kwenye Twitter mwaka 2013. “Ana miezi miwili tu! Ni wa kike lakini nimemwita SUPER!).” 

Balotelli aliwavutia mashabiki wengi na uhusiano wake huu wa kipekee. Hata hivyo, alipohamia Liverpool, Super alizuiwa kuingia Uingereza, jambo ambalo lilisababisha majonzi kwa mshambuliaji huyo.


WNY03
WNY03

ROY KEANE

Roy Keane, ambaye mara nyingi amejulikana kwa ukali wake uwanjani, maisha yake ya nje ya uwanja ni mtu tofauti kabisa, ana upande laini ambao hujitokeza pale anapokuwa karibu na mbwa wake. Mbwa wake maarufu, Triggs, alikumbukwa sana wakati wa Kombe la Dunia 2002, alipokuwa sehemu ya mgogoro wa kihistoria kati ya Keane na timu ya taifa ya Ireland. 

“Tofauti na watu, mbwa hawasemi upuuzi,” alisema Keane kuhusu Triggs katika kitabu cha maisha ya mbwa huyo. 

Baada ya Triggs kufariki mwaka 2012, Keane ameendelea kufuga mbwa wengine. Keane pia ni balozi wa Irish Guide Dogs, akionyesha wazi umuhimu wa mbwa katika maisha yake na jamii.


WNY01
WNY01

ALEXIS SANCHEZ 

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United, Alexis Sanchez amekuwa maarufu kwa mapenzi yake ya dhati kwa mbwa wake wawili, Atom na Humber. Mbwa hawa walipata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wakati akicheza Ligi Kuu England. 

“Atom ni jina la mhusika katika filamu Real Steel,” alieleza Sanchez. “Atom ni mzee na anaonekana hana nguvu, lakini anapopigana, huwashinda roboti bora duniani. Humber, kwa upande mwingine, alinipa kumbukumbu ya kaka yangu Humberto. Ni mpole na mtiifu kama mbwa wangu.” 

Hata baada ya kuondoka Arsenal, Sanchez ameendelea kuonyesha mapenzi kwa Atom na Humber, ambao wamekuwa sehemu muhimu ya maisha yake. 


KYLE WALKER NA JOHN STONES

Wakati wachezaji wengi wanapendelea mbwa, Kyle Walker na John Stones wa Manchester City walihusudu paka wa mitaani aliyeonekana kwa bahati nchini Qatar wakati wa Kombe la Dunia 2022. 

Paka huyo, aliyepewa jina Dave, alitembelea mara kwa mara kambi ya mazoezi ya timu na kuwa kipenzi cha wachezaji hao wawili. Walker alisema: “Alionekana tu siku moja, na tukamchukua mimi na Stoney.” 


MEMPHIS DEPAY

Memphis Depay, anayejulikana kwa tattoo kubwa ya simba mgongoni mwake, pia anaonyesha upendo mkubwa kwa simba halisi. Kitabu chake cha maisha, Heart of a Lion, kinaonyesha jinsi alivyopata msukumo wa ujasiri na nguvu kutoka kwa wanyama hawa. Depay amekuwa balozi wa wanyama pori, akihamasisha uhifadhi wa simba kupitia shughuli mbalimbali za kijamii.


CLAUDIO PIZARRO

Mapenzi ya Claudio Pizarro kwa farasi ni ya kipekee. Nyota huyu wa zamani wa Bayern Munich na Chelsea amewekeza sana katika farasi, akiwa nao zaidi ya 50 huko Amerika Kusini. 

Alishirikiana hata na Joey Barton kumiliki farasi aliyepewa jina Crying Lightning, jina lililotokana na wimbo wa Arctic Monkeys. “Nilipenda farasi tangu nikiwa mtoto na niliwaita majina ya miji na wachezaji wa Ujerumani kama Don Jupp na Uli Hoeness,” alisema Pizarro.