Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msiba wa Papa waahirisha mechi za ligi Italia

Papa Pict

Muktasari:

  • Papa Francis amefariki dunia, Jumatatu, Aprili 21 akiwa na umri wa miaka 88.

Taarifa iliyotolewa na bodi ya Ligi Kuu Italia leo, imeeleza kwamba mechi hizo zitapangiwa tarehe nyingine badala ya kuchezwa leo.

“Kutokana na kifo cha Mtakatifu, Serie A inathibitisha leo kwamba mechi za ligi za Serie A na Primavera 1 zimeahirishwa. Tarehe ambayo zitapangwa zitatangazwa hivi karibuni,” imefafanua taarifa hiyo.

Mechi nne za Ligi Kuu ya Italia ambazo zimeahirishwa ni kati ya Torino na Udinese, Cagliari na Fiorentina, Genoa na Lazio na Parma na Juventus.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki na Vatican alizaliwa Desemba 17, 1936 jijini Buenos Aires, Argentina na kubatizwa jina la Jorge Mario Bergoglio.

Mapema leo asubuhi, Vatican ilitangaza kifo cha Papa Francis.

Kwa mujibu wa Vatican, tangazo la Camerlengo Kardinali Farrell kutoka nyumba ya Mtakatifu Marta imesema:

"Saa 1:35 asubuhi ya leo Jumatatu Aprili 21, Askofu wa Roma, Francisko alirudi kwenye nyumba ya Baba. Maisha yake yote yaliwekwa wakfu kwa huduma ya Bwana na Kanisa."

Kardinali Kevin Farrell alitangaza kifo cha Papa akisema:

"Kaka na dada wapendwa ni kwa huzuni kubwa kwamba sina budi kutangaza kifo cha Baba yetu Mtakatifu Francisko. Saa 1:35 asubuhi ya leo, (Jumatatu Aprili 21, 2025), Askofu wa Roma, Francisko, alirejea nyumbani kwa Baba."

Amesema maisha yake yote yaliwekwa wakfu kwa huduma ya Bwana na kanisa lake.

"Alitufundisha kuishi maadili ya Injili kwa uaminifu, ujasiri na upendo wa ulimwengu wote, hasa kwa kupendelea maskini zaidi na waliotengwa zaidi. Kwa shukrani nyingi kwa ajili ya kielelezo chake kama mfuasi wa kweli wa Bwana Yesu, tunaiweka roho ya Papa Francisko kwa upendo wa huruma usio na kikomo wa Mungu mmoja na wa Utatu," amesema.