Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mustakabali wa Pulisic AC Milan shakani, mazungumzo yasimama

PURiSIC Pict

Muktasari:

  • Zaidi ya masuala ya uwanjani, kipengele muhimu kinaweza kuwa kodi ikizingatiwa kwamba sheria ya Italia inayojulikana kama “Growth Decree”, Pulisic anaweza kuendelea kupata faida kubwa za kikodi ikiwa atasaini mkataba mpya hata kuongeza hadi miaka mingine mitano iwapo atawekeza katika mali isiyohamishika nchini humo.

MILAN, ITALIA: MAZUNGUMZO ya kuongeza mkataba ya winga wa AC Milan, Christian Pulisic na timu yapo shakani yakiwa yamesimama kwa sasa kutokana na kushuka kwa kiwango chake cha uchezaji, matatizo ya kimwili na mvutano fulani kutoka upande wa mchezaji.

Hata hivyo, bado kuna nia ndani ya klabu hiyo kurekebisha hali hiyo, ambapo kiwango cha Pulisic kimeporomoka msimu huu. Baada ya kuanza msimu kwa kiwango cha juu akifunga wastani wa bao kila dakika 74, Mmarekani huyo hajafunga tangu Desemba 28, mwaka jana dhidi ya Hellas Verona.

Tangu hapo, amecheza zaidi ya mechi 10 bila kufunga, ambapo asisti yake ya hivi karibuni dhidi ya Torino imekuwa kama nafuu tu katikati ya kipindi kigumu kilichozua mashaka kwa mashabiki na wachambuzi wa soka wa Italia.

Hata hivyo, anaungwa mkono ndani ya kikosi. Wachezaji wenzake kama Youssouf Fofana na Adrien Rabiot wameonyesha kumuunga mkono.

Nje ya uwanja, Pulisic anaishi maisha ya utulivu akiepuka vyombo vya habari jijini Milan na kuchagua kuishi maeneo tulivu ya Busto Arsizio akiwa anapenda zaidi kucheza gofu na muziki, na ameepuka kuchochea uvumi kuhusu mustakabali wake.

Mchezaji huyo amekaririwa akisema: "Sizungumzi na wakala wangu kuhusu klabu au kuondoka. Nina furaha hapa na ninazingatia kucheza."

Zaidi ya masuala ya uwanjani, kipengele muhimu kinaweza kuwa kodi ikizingatiwa kwamba sheria ya Italia inayojulikana kama “Growth Decree”, Pulisic anaweza kuendelea kupata faida kubwa za kikodi ikiwa atasaini mkataba mpya hata kuongeza hadi miaka mingine mitano iwapo atawekeza katika mali isiyohamishika nchini humo.

Mtihani ujao dhidi ya Napoli katika Uwanja wa Stadio Diego Armando Maradona unaweza kuwa nafasi nzuri kwake kurejea kwenye kiwango bora, na katika kipindi ambacho mustakabali wake haujulikani, kila mechi ina uzito mkubwa. AC Milan wanatumaini kumrejesha nahodha huyo wa Marekanin uwanjani wakati wakifanya jitihada za kufufua mazungumzo ya mkataba ambayo kwa sasa yamesimama.