Pauni 253 mil zakaa benchi

Hadi jana, nyota hao wenye thamani ya Pauni 253.2 milioni walikuwa majeruhi
Muktasari:
- Idadi kubwa ya majeruhi imepunguza kasi ya baadhi ya timu na kusababisha kupata matokeo mabaya
London, England. Licha ya klabu 20 za Ligi Kuu England kutumia pauni 630 milioni kuimarisha vikosi vyao, klabu hizo zimepata pigo baada ya nyota hao kuwa majeruhi.
Hadi jana, nyota hao wenye thamani ya Pauni 253.2 milioni walikuwa majeruhi, kiasi cha kukosa mechi kuanzia zilizochezwa mwisho wa wiki.
Orodha hiyo ya nyota majeruhi na wakati wao wa kurudi dimbani kwa klabu 20 pamoja na thamani zao kwenye mabano:
Arsenal
Alex Oxlade-Chamberlain (goti) – Desemba 13 (Pauni 15 mil), Lukas Podolski (Kano) – Desemba 7 (Pauni 10.9 mil), Mikel Arteta – (Papa/kiuno) – Septemba 28 (Pauni 10 mil), Abou Diaby (goti) – Haijulikani (Pauni 2 mil), Thomas Vermaelen (Mgongo) – Septemba 28 (Pauni 10 mil),Tomas Rosicky (Paja) – Haijulikani (Pauni 12 mil) Yaya Sanogo (mgongo) – Septembar 14 (huru) Jumla: Pauni 59.9 milioni
Aston Villa
Charles N’Zogbia (misuli) – Mwishoni mwa 2013 (Pauni 9.5 mil) Jumla: Pauni 9.5 mil Cardiff City Andreas Cornelius (enka) – Septemba 14 (Pauni 7.5 mil) Jumla: Pauni 7.5 mil
Chelsea
Oscar (Enka) – Septemba 14 (Pauni 25 mil) Tomas Kalas (Mguu umevunjika) – Haijulikani (Pauni 5.2 mil) Jumla: Pauni 30.2 milioni
Crystal Palace
Glenn Murray (Goti) – Haijulikani – (Huru) Jerome Thomas (Enka) – Septemba 14 (huru) Jack Hunt (Mguu umevunjika) – Haijulikani (Pauni 2 mil) Jonny Williams (Enka) – Hakuna muda maalumu (Kikosi B) Patrick McCarthy (hana mazoezi) (huru) Jonathan Parr (Hana mazoezi) (ada yake siri) Yannick Bolasie (kifundo) – Haijulikani (ada yake siri) Jimmy Kebe (nyonga) – Haijulikani (ada yake siri) Jumla: Pauni 2 mil
Everton
Antolin Alcaraz (kifundo) – Septemba 21 (huru) Jumla: 0
Fulham
Kieran Richardson (Kifundo) – Septemba 21 (Pauni 2 mil) Maatern Stekelenburg (Bega) – Haijulikani Pauni 4.3 mil) Aaron Hughes (Paja) – Septemba 14/21 ( pauni 1 mil) Jumla: Pauni 7.3 mil
Hull
Abdoulaye Faye (Kano) – Septemba 14 (huru) George Boyd (enka) – Septemba 14 (huru) Allan McGregor (nyonga) – Septemba 14/21 (Pauni 1.8 mil)Jumla: Pauni 1.8 mil
Liverpool
Daniel Sturridge (paja) – Septemba 14/21 (Pauni 12 mil) Glen Johnson (enka) –Siyo mbaya (Pauni 17.5 mil) Joe Allen (kifundo) – Septemba 14/21 (Pauni 15 mil) Kolo Toure (nyonga) – Septemba 14/21 (huru) Aly Cissokho (Enka) – Oktoba 12 (Mkopo) Sebastian Coates (Goti) – Mei 2014 (Pauni 7 mil)Jumla: Pauni 51.5 mil
Man United
Rafael (kifundo) – Septemba 14 (Pauni 5.2 mil, yeye na Fabio) Wayne Rooney (kichwa) – Septemba 21 (Pauni 27 mil) Phil Jones (enka) – Haijulikani (Pauni 16 mil) Darren Fletcher – Haijulikani (KikosiB) Jumla Pauni 48.2 mil
Man City
David Silva (Enka) – Septemba 14 (Pauni 24 mil) Vincent Kompany (nyonga) – Oktoba 5 (Pauni 6 mil) Martin Demichelis (Goti) – Oktoba 26 (Pauni 3.8 mil) Micah Richards (kifundo) – Septemba 14 (Kikosi B) Jumla: Pauni 33.8 mil
Newcastle
Mike Williamson (maungo) – Septemba 14 (Pauni 2 mil)Ryan Taylor (Goti) – Haijulikani (Pauni 6 mil) Jonas Gutiérrez (kifundo) – Septemba 14/21 (Siri) Gabriel Obertan (kifundo) – Septemba 14 (Pauni 3 mil) Jumla: Pauni 11 mil
Norwich
- Ryan Bennett (maungo) – Septemba 14/21 (Pauni 3.2 mil) Elliott Bennett (goti) – Haijulikani (siri) Gary Hooper (mfupa) – Septemba 14 (Pauni 5 mil) Jumla: Pauni 8.2 mil
Tottenham
Etienne Capoue (Enka) – Septemba 28 (Pauni 8.6m) Aaron Lennon (Enka) - Septemba 14 (Pauni 1m) Jumla: Pauni 9.6m