Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rabiot apambana Pogba kutua Marseille

Muktasari:

  • Pogba ambaye alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake na Juventus, pia amekuwa akitajwa anaweza kurudi England pia.

MARSEILLE inataka kuanza mazungumzo na wawakilishi wa kiungo raia wa Ufaransa, Paul Pogba ili kumsajili mwakani mara baada ya adhabu yake ya kufungiwa kutokana na kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni kumalizika ifikapo Machi.

Pogba ambaye alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake na Juventus, pia amekuwa akitajwa anaweza kurudi England pia.

Inaelezwa mmoja kati ya mastaa wanaopambana kuhakikisha Pogba anatua  Marseille ni Adrien Rabiot ambaye amejiunga na timu hiyo dirisha lililopita.

Rabiot ambaye ni rafiki wa karibu wa Pogba ndiye anatumika kama kishawishi cha Mfaransa huyo kutua Marseille ambayo kwa sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligue 1.

Hivi karibuni Pogba pia alionekana Marekani akiwa pamoja na mlinzi wa Lionel Messi hali iliyoibua ripoti anaweza akatua Inter Miami.


ARSENAL imeshaanza mchakato wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Serbia, Dusan Vlahovic dirisha lijalo la majira ya baridi ili kuboresha eneo lao la ushambuliaji. Licha ya matokeo mazuri iliyopata katika mechi zilizopita, bado Mikel Arteta anaamini timu hiyo inahitaji mshambuliaji bora zaidi. Mkataba wa Vlahovic unamalizika mwaka 2026 na mbali na Washika mitutu hao, Chelsea pia imeonyesha nia ya kuhitaji saini yake.


LICHA ya kutoonyesha kiwango bora, ripoti kutoka tovuti ya Standard zimefichua kocha Mikel Arteta hana mpango wa kutoa ruhusa ya kuuzwa kwa straika wa timu hiyo na Brazil, Gabriel Jesus ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Jesus mwenye umri wa miaka 27, msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote na kufunga bao moja tu na amekuwa akikosa baadhi ya mechi kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.


BEKI wa kati wa Liverpool na Uholanzi, Virgil van Dijk, yupo tayari kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye timu hiyo licha ya kudaiwa kukataa ofa ya kwanza iliyowekwa mezani. Van Dijk mwenye umri wa miaka 33, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu. Liverpool inataka kumsainisha mkataba mpya kwa sababu ni mmoja kati ya wachezaji wao tegemeo wa kikosi cha kwanza.


NEWCASTLE United ipo katika mazungumzo ya kumsajili winga wa PSV Eindhoven na Ubelgiji, Johan Bakayoko, 21, katika dirisha lijalo. Tangu kuanza kwa msimu huu, Newcastle imekuwa katika hali mbaya na moja ya maeneo ambayo benchi la ufundi linaona yana waangusha ni lile la ushambuliaji. Msimu huu Bakayoko amecheza mechi 21 za michuano yote na kufunga mabao sita.


MAZUNGUMZO ya Liverpool na staa wao raia wa Misri,  Mohamed Salah, 32, juu ya mkataba mpya yapo hatua za mwisho na sasa kinachojadiliwa ni muundo wa malipo yake ya bonasi ya usajili na mshahara. Awali jambo lililokuwa linakwamisha ni urefu wa mkataba na Salah alikuwa akihitaji miaka mitatu wakati Liverpool ikihita kumpa mmoja. Sasa atasaini miaka miwili.


AC Milan ipo tayari kumruhusu beki na kapteni wao, Theo Hernandez kuondoka dirisha lijalo la majira ya baridi lakini kwa timu itakayokuwa tayari kulipa Pauni 41 milioni. Theo mwenye umri wa miaka 27, ana uwezo mkubwa wa kucheza kama beki wa kushoto na amekuwa akiwindwa na vigogo mbalimbali ikiwa pamoja na Manchester United na Real Madrid.


CHELSEA haina mpango wa kumtoa kwa mkopo beki wao wa kati raia wa England, Tosin Adarabioyo,  katika dirisha lijalo la majira ya baridi na anahusishwa na West Ham. Adarabioyo mwenye umri wa miaka 27, anahusishwa kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Chelsea tangu atue ktika dirisha lililopita.