Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ramires alivyoshtua watu kwa mwonekano wake

RAMIRES Pict

Muktasari:

  • Kama ni kweli au sikweli, hivi umeshawahi kumwona staa wa zamani wa Chelsea, kiungo wa Kibrazili, Ramires kwa siku za karibuni?

LONDON, ENGLAND: KUNA huu msemo, eti unaanza kuzeeka kwanza kabla ya kuwa kijana.

Kama ni kweli au sikweli, hivi umeshawahi kumwona staa wa zamani wa Chelsea, kiungo wa Kibrazili, Ramires kwa siku za karibuni?

Nyota huyo wa The Blues aliwashangaza mashabiki wake kutokana na mwonekano wake wa sasa, umemfanya ashindwe kutambulika kabisa. Ramires aliichezea Chelsea mechi 251 kati ya mwaka 2010 na 2016, akifunga mabao 34 na asisti 17.

Alijiunga na klabu hiyo ya Stamford Bridge akitokea Benfica kwa ada ya Pauni 17 milioni na alikuwa akivaa jezi Namba 7.

RAMI 01

Moja ya tukio lake bora kabisa akiwa Chelsea ni bao lake la dakika za majeruhi kwenye kipindi cha kwanza dhidi ya Barcelona kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012 na ilikuwa mechi ya marudiano iliyofanyika uwanjani Camp Nou.

Mbrazili huyo alikimbia na kufunga bao kwa mpira wa kuchopu kumpita kipa Victor Valdes na iliisaidia Chelsea kusawazisha kwenye mabao ya jumla.

Fernando Torres kisha alifunga bao kwenye dakika za majeruhi za kipindi cha pili kuifanya Chelsea kuongoza 3-2 kwenye matokeo ya jumla na kutinga fainali, ambako ilikwenda kuichapa Bayern Munich na kubeba taji hilo.

Hata hivyo, kwenye mechi hiyo Ramires alionyeshwa kadi ya njano ambayo ilimfanya akose fainali, licha ya kwamba mchango wake haukuwahi kusahaulika. Sasa, akiwa na umri wa miaka 37, Ramires amekuwa na mwonekano tofauti kabisa na alivyokuwa akicheza Chelsea.

RAMI 02

Ramires alistaafu soka akiwa na kikosi cha Palmeiras mwaka 2020 na baada ya hapo, amekuwa tofauti kabisa na kuwashangaza watu, alipotinga tena uzi wa The Blues kwenye uwanja wa mazoezi wa Cobham.

Na jambo hilo liliwafanya mashabiki kusema, ambapo shabiki wa kwanza alisema: "Niwe mkweli jamani, huyu ni nani?" Shabiki wa pili alisema: "Nani??"

Shabiki wa tatu alisema: "Gwiji ameshindwa kutambulika kabisa."

Mwingine alisema: "Ramires amebadilika sana."

RAMI 03

Ramires aliungana kwa ajili ya mechi ya magwiji sambamba na mastaa wengine John Obi Mikel, Claude Makelele, William Gallas, Jimmy Floyd Hasselbaink na Roberto Di Matteo, ambaye amerudi kwenye kikosi kama kocha.