Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid haina papara kwa Alexander Arnold

Arnord Pict

Muktasari:

  • Madrid inataka kufanikisha dili la Trent kama ilivyokuwa kwa Mbappe ambaye kiasi kikubwa cha pesa inamlipa kupitia bonasi ya usajili.

LIVERPOOl, ENGLAND: BAADA ya juzi, Liverpool kudaiwa kukataa ofa ya Pauni 20 milioni kutoka kwa Real Madrid iliyokuwa ikihitaji saini ya beki wao wa kulia Trent Alexander Arnold, katika dirisha hili, sasa timu hiyo imepanga kusubiri hadi mwisho wa msimu ili kumsajili atakapokuwa huru ambapo imepanga kumpa mpunga wa kutosha utakaoweza kumfanya kuwa mchezaji wa pili kwa kulipwa zaidi barani Ulaya baada ya Kyalian Mbappe.

Madrid inataka kufanikisha dili la Trent kama ilivyokuwa kwa Mbappe ambaye kiasi kikubwa cha pesa inamlipa kupitia bonasi ya usajili.

Kijumla pesa ambazo Madrid imepanga kumpa Trent zitazidi kumfanya awe tajiri kwani mbali ya mshahara mkubwa utakaozidi ule wa Pauni 180,000 kwa wiki anaoupata hivi sasa akiwa na Liverpool, Madrid itamwekea pia Pauni 100 milioni katika mkataba wake ambayo itamlipa katika kipindi cha miaka atakayosaini.

Hii ni sawa na Mbappe ambaye mbali ya mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki anaoupata, Madrid pia inamumeweka Pauni 128 milioni ambayo inamlipa katika kipindi cha miaka mitano ya mkataba wake.

Ingawa Trent haonekani kama atafikia mkwanja sawa na ule ambao Mbappe anaupata, kiasi kinachotarajiwa kuwekwa kinaweza kukaribiana na kile cha Mbappe.

Ripoti kutoka Hispania zinaeleza Trent ambaye ni zao la akademi ya Liverpool akiwa katika kikosi hicho tangu ana umri wa miaka sita, amewaambia mabosi wa Anfield kuwa anataka kuondoka baada ya kudumu kwa miaka 20 kwenye timu hiyo.

Hata hivyo, Liverpool imekanusha juu ya taarifa hiyo na sasa inapambana kumshawishi abaki katika kikosi kwa msimu ujao.

Mbali ya mshahara wake, staa huyu anadaiwa kuwa atakuwa akiishi eneo la La Finca katika kitongoji cha Pozuelo de Alarcon, ambako wachezaji wengi mastaa wa Madrid wanaishi.

Hapo ndipo Gareth Bale alipoishi kwa miaka mingi pamoja na Cristiano Ronaldo na Karim Benzema pia hivi sasa Kylian Mbappe yupo hapo. Hakuna taarifa kama atapewa mjengo wa kuishi bure ama pesa ya nyumba itajumuishwa katika mshahara wake. Mbali ya Trent, Madrid pia inahitaji huduma ya beki tegemeo wa kikosi cha Arsenal na  Ufaransa, William Saliba ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

Hata hivyo, mwezi uliopita staa huyu alikanusha taarifa za yeye kuwa katika mpango wa kuondoka alipoulizwa swali kuhusiana na tetesi hizo.

“Ninajihisi niko nyumbani hapa. Nimesaini na timu hii miaka mitano uliyopita na huu ni msimu wangu wa tatu na ninainjoi maisha na kila kitu, nina furaha juu ya mashabiki, wachezaji wenzangu na viongozi wa timu, ningependa kubaki hapa.”