Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo amaliza ubishi wa Messi

Muktasari:

  • Moja kati ya mataji ambayo Ronaldo hana ni lile la Kombe la Dunia ambalo Messi alilichukua mwaka 2022 akiwa na timu ya taifa ya Argentina katika mashindano yaliyofanyika nchini Qatar.

RIYADH, SAUDI ARABIA: STAA wa Al Nassr na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amesema mjadala wa yeye na Lionel Messi juu ya nani bora hautokoma hata akifanikiwa kuchukua taji la Kombe la Dunia.

Moja kati ya mataji ambayo Ronaldo hana ni lile la Kombe la Dunia ambalo Messi alilichukua mwaka 2022 akiwa na timu ya taifa ya Argentina katika mashindano yaliyofanyika nchini Qatar.

Ronaldo ambaye amewahi kushinda taji la Euro akiwa na Ureno mwaka 2016 walipocheza fainali dhidi ya Ufaransa, lengo lake kwa sasa ni kushinda Kombe la Dunia akiwa na taifa hilo ingawa anaamini bado haitabadilisha uelekeo wa ubishani unaoendelea juu ya nani bora kati yake na Messi.

“Hata nikishinda Kombe la Dunia, hiyo itaendelea kuwa hivyo. Baadhi ya watu wananipenda sana na wengine wananipenda kwa wastani na wengine hawanipendi kabisa. Ni kama katika maisha tu, kila mtu ana kitu chake anachokipenda.

“Daima nililazimika kuonyesha kile niwezacho kufanya mwaka baada ya mwaka. Ningependa kushinda mashindano haya (Kombe la Dunia), nina hamu ya kutwaa lakini ikiwa nitashindwa bado nitakuwa na furaha kwa mataji ambayo nimeshinda hadi sasa,  katika vitabu vya historia, rekodi nyingine zote zitakuwa hapo.”

Ronaldo anaweza kuwa na nafasi moja zaidi ya kushinda Kombe la Kombe la Dunia ikiwa atachaguliwa na kocha Roberto Martinez kwenye kikosi cha Ureno kitakachoshiriki   WC 2026.