Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot lazima avunje benki kwa Khvicha

Muktasari:

  • Kocha Arne Slot ni wazi kabisa anahitaji huduma ya winga huyo fundi wa boli kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya kuona mpango wao wa kumchukua staa wa Newcastle United, Anthony Gordon unahitaji pesa nyingi ili kumpata Mwingereza huyo.

LIVERPOOL, ENGLAND: NDO hivyo. Liverpool italazimika kuvunja rekodi yake uhamisho kama kweli inataka kukamilisha dili la kupata huduma ya winga wa Georgia, Khvicha Kvaratskhelia kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Kocha Arne Slot ni wazi kabisa anahitaji huduma ya winga huyo fundi wa boli kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya kuona mpango wao wa kumchukua staa wa Newcastle United, Anthony Gordon unahitaji pesa nyingi ili kumpata Mwingereza huyo.

Licha ya ukweli kwamba Luis Diaz, Cody Gakpo, Diogo Jota na Mohamed Salah wataendelea kubaki Anfield hadi msimu ujao, bado kuna mpango wa kuongeza silaha mpya ili kumpa kocha Slot machaguo ya kutosha kwenye timu yake.

Staa wa Napoli, Kvaratskhelia ni jina linalopewa nafasi kubwa na mabosi wa Anfield na wanadhani litakuwa chaguo bora zaidi katika maandalizi ya kupata mchezaji wa kuja kuchukua mikoba ya Mo Salah.

Baba yake Kvaratskhelia aliiambia Calcio Napoli 24: “Ni kitu kizuri kumlinganisha na Mo Salah kwa sababu ni mchezaji mahiri na amefanya mambo makubwa Liverpool na Misri. Lakini, Khvicha yupo vizuri zaidi. Wengi wanasema ana nguvu zaidi. Kwa upande wangu, naunga mkono hilo pia, si tu kwa sababu mimi ni baba yake, bali kwa kuwasikia wengi wakisema juu ya jambo hilo.’

Beki wa zamani wa Liverpool, Markus Babbel alisema: “Khvicha Kvaratskhelia ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu na kama kutakuwa na nafasi ya kuja Liverpool itakuwa safi sana kwa sababu anaweza kufiti kwenye namna ambavyo timu inacheza.

“Nadhani itakuwa vizuri pia kwake. Ni mjanja, anataka mpira muda wote. Atazitesa timu kwa kasi yake na hiyo ndiyo staili ya soka la Liverpool. Atakuwa ingizo bora kabisa kwenye Ligi Kuu England kwa sababu umri wake ndiyo kwanza miaka 23. Lakini, sidhani kama rais wa Napoli atafanya mambo kuwa mepesi. Kama ataondoka, basi itakuwa kwa dau la Pauni 150 milioni, pesa ambayo ni nyingi sana kwa Liverpool.”

Ripoti zinadai kwamba PSG ilijaribu kumnasa staa huyo, Kvaratskhelia, lakini ofa yao ya Pauni 111 milioni ilikataliwa na Napoli.