Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuchel amkumbusha Kane yeye ni straika

Muktasari:

  •  Tuchel, ambaye alimsajili Kane kutoka Tottenham Hotspur wakati alipokuwa akiinoa Bayern Munich mwaka 2023, anafahamu kilichofanya straika huyo akosolewe ni kutokana na kushuka chini na kucheza kwenye kiungo wakati wa Euro 2024.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa England, Thomas Tuchel amesema anatarajia kumwona straika Harry Kane kucheza eneo la kushambulia na si kwenye safu ya kiungo kama ambavyo alikuwa akitumika huko nyuma kwenye baadhi ya mechi za kikosi cha Three Lions.

Tuchel, ambaye alimsajili Kane kutoka Tottenham Hotspur wakati alipokuwa akiinoa Bayern Munich mwaka 2023, anafahamu kilichofanya straika huyo akosolewe ni kutokana na kushuka chini na kucheza kwenye kiungo wakati wa Euro 2024.

Kane, 31, ambaye amefunga mabao 69 katika mechi 103 alizochezea England, ametikisa nyavu mara 32 huko Bayern msimu huu.

Tuchel alisema: “Nafahamu Harry ni mshambuliaji, ni mchezaji wa kulipwa ambaye yupo tayari kufanya chochote anachotakiwa kufanya na anafanya hivyo akiwa na Bayern kwa sasa. Wao wanacheza kwa staili ya kukabia juu - ni kama vile wanakaba mtu na mtu.

“Nilimwona hapa England alikuwa akishuka chini kabisa kwenye mechi, pengine hivyo sivyo tunavyotaka Harry afanye. Kumfanya ashuke kama Namba 9 si tatizo, lakini sio ashuke hadi kwenye Namba 6. Akishuka kama Namba 10, kupata nafasi ya kupiga mashuti na kuliona vizuri goli akiwa nje ya boksi, hilo si tatizo.

“Lakini, tunahitaji pia kuwa na watu wenye kasi kumzunguka ili aweze kutumia nafasi. Tuna matarajio makubwa kutoka kwake tunapomchezesha. Yeye ni nahodha wetu. Sio mtu mzungumzaji sana, lakini tunatarajia makubwa kwake.”

Tuchel pia amepanga kusafiri hadi Saudi Arabia kumtazama straika Ivan Toney, licha ya kwamba safari hii hajamjumuisha kwenye kikosi chake kutokana na kumuita mshambuliaji wa Spurs, Dominic Solanke. Tuchel amemrudisha pia kwenye kikosi Marcus Rashford.