Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usajili mpya 2025 mjadala England

USAJILI Pict

Muktasari:

  • Dirisha la usajili la majira ya kiangazi la mwaka jana lilifungwa Agosti 31, 2024, na hili la mwaka huu litafunguliwa rasmi Juni 12. Hata hivyo, mpango mpya wa dirisha la mwaka huu ni kufungwa Agosti 14, siku mbili kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu England 2025/26.

LONDON, ENGLAND: MABOSI wa Ligi Kuu England wanajiandaa kufanya mazungumzo ya kubadili siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi mwaka huu, imeelezwa.

Dirisha la usajili la majira ya kiangazi la mwaka jana lilifungwa Agosti 31, 2024, na hili la mwaka huu litafunguliwa rasmi Juni 12. Hata hivyo, mpango mpya wa dirisha la mwaka huu ni kufungwa Agosti 14, siku mbili kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu England 2025/26.

Mpango huo ulianza kujadiliwa mapema mwezi uliopita kwenye mkutano wa wakurugenzi wa michezo wa klabu za Ligi Kuu England na hautakuwa mpya kwani uliwahi kutumika kabla ya kufutwa mwaka 2018 na 2019.

Hiyo ina maana usajili kama wa kiungo Manuel Ugarte huko Manchester United, aliyenaswa zikiwa mechi mbili zimeshafanyika Ligi Kuu England huko nyuma usingetokea.

Mabosi wa klabu watajadili mpango huo kwenye kikao kitakachofanyika Alhamisi hii. Ili mabadiliko hayo kupitisha yatahitaji kura za klabu 14, licha ya kwamba kama mjadala wa awali utaonekana kukosa sapoti, unaweza kumalizwa kabla ya kusubiri kipengele cha kupiga kura. Mpango wa wakurugenzi wa michezo wa klabu kumaliza biashara zote za usajili kabla ya ligi kuanza Agosti 16.

Kingine cha ziada kwenye mjadala huo ni kupunguza usajili wa dirisha la Januari hadi kuwa wa wiki mbili tu ili kupunguza usumbufu wa kikosi kwa kuwa usajili huo unakuwa unafanyika katikati ya msimu.

Tatizo moja kubwa kwenye mpango huo ni kuzishawishi ligi za nchi nyingine za Ulaya kukubali kuunga mkono hilo. Tishio jingine pia ni Saudi Pro League, ambayo imekuwa ikitoa pesa nyingi kufanya usajili baada ya Ligi Kuu England. Kwamba klabu za Ligi Kuu England zinaweza kuwa zimeshafunga usajili, wakati ligi nyingine bado zinasajili na kutua humo kubeba mastaa wao.

Huko nyuma, timu zilikuwa zinaruhusiwa kusajili muda wote wa msimu, ambapo usajili mkubwa kama wa Eric Cantona kwenda Man United ulifanyika Novemba 25, kipindi hicho na Man United ilikuwa ishacheza mechi 16 kwenye ligi.