Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UTAIPENDA: Brazil

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Brazil wakishangilia ushindi dhidi ya timu ya Taifa ya Cameroon.

Muktasari:

  • Brazil waliandika bao la kwanza katika dakika ya 16 lililofungwa na staa wao Neymar aliyeitumia vizuri krosi ya Luiz Gustavo.

BRASILIA, BRAZIL

WENYEJI Brazil jana Jumatatu walifuzu kwa kishindo hatua ya pili ya fainali za Kombe la Dunia baada ya kuilaza Cameroon mabao 4-1 na kushika usukani katika Kundi A wakiwa na pointi saba.

Brazil waliandika bao la kwanza katika dakika ya 16 lililofungwa na staa wao Neymar aliyeitumia vizuri krosi ya Luiz Gustavo.

Cameroon ambao waliziaga rasmi fainali hizo walisawazisha bao hilo dakika 10 baadaye mfungaji akiwa Joel Matip aliyemalizia kazi nzuri iliyofanywa na Allan Nyom.

Hata hivyo dakika 10 kabla ya timu kwenda mapumziko, Neymar aliwainua vitini mashabiki wa Brazil alipofunga bao la pili akiitumia vizuri pasi ya Marcelo.

Dakika ya 49, Brazil waliongeza bao la tatu lililofungwa kwa kichwa na Fred ambaye aliunganisha krosi ya David Luiz.

Bao la nne la Brazil lilipatikana dakika ya 84 mfungaji akiwa ni Fernandinho aliyeinasa pasi ya Oscar na kuujaza mpira wavuni.

Nayo Mexico inaungana na Brazil katika hatua ya pili ya michuano hiyo kutoka Kundi A baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Croatia na kufikisha pointi saba sawa na Brazil.

Mabao ya Mexico yalifungwa na Rafael Marquez, Andrés Guardado na Javier Hernández ‘Chicharito wakati bao pekee la Croatia lilifungwa na Ivan Perisic.

Baada ya kufuzu hatua ya pili inayoshirikisha timu 16, Brazil sasa itaumana na Chile Jumamosi ijayo wakati Mexico itaumana na Uholanzi siku inayofuata.

Uholanzi ilimaliza mechi zake za Kundi B jana kwa kishindo baada ya kuilaza Chile mabao 2-0 na kushika usukani wa kundi hilo wakiwa na pointi 9.

Mabao ya washindi yaliyopatikana kipindi cha pili yalifungwa na Leroy Fer na Memphis Depay.

Nayo Hispania iliziaga fainali hizo kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Australia katika mechi nyingine ya Kundi B, mabao ya washindi yalifungwa na David Villa, Fernando Torres na Juan Mata. Chile iliyofikisha pointi sita na Uholanzi ndizo zilizofuzu kundi hilo.

Mechi za fainali hizo zitakazopigwa leo Jumanne ni kama ifuatavyo...

Italia v Uruguay, Costa Rica v England, Ugiriki v Ivory Coast na Japan v Colombia.