Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yamal kuharibu mipango ya Arsenal

YAMAL Pict
YAMAL Pict

Muktasari:

  • Nico ambaye anawindwa na vigogo wengi barani Ulaya, anadaiwa kuwa ni rafiki mkubwa wa Yamal jambo ambalo mabosi wa Barca wanaamini ni kama fursa ya kushinda vita dhidi ya timu nyingine kwani watamtumia staa huyo kushawishi.

BARCELONA, HISPANIA: STAA wa Barcelona, Lamine Yamal anadaiwa kuwa kutibua mipango ya Arsenal katika harakati za kutaka kumsajili winga wa Athletic Bilbao na timu ya taifa ya Hispania, Nico Williams kwenye dirisha lijalo.

Nico ambaye anawindwa na vigogo wengi barani Ulaya, anadaiwa kuwa ni rafiki mkubwa wa Yamal jambo ambalo mabosi wa Barca wanaamini ni kama fursa ya kushinda vita dhidi ya timu nyingine kwani watamtumia staa huyo kushawishi.

Barca ilijaribu kumsajili winga huyo katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana baada ya mchango wake katika michuano ya Euro 2024 akiwa na timu ya taifa ya Hispania, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 aliamua kubaki ili kupata uzoefu zaidi.

Hata hivyo, Barca haijakata tamaa ya kumsajili mchezaji huyo na itarudi tena mezani katika dirisha lijalo huku ikiwa na ushawishi wa Yamal.

Arsenal pia inataka kulipa Euro 60 milioni ambazo zimewekwa katika mkataba wake kwa timu inayotaka kumsajili, lakini kabla ya kiasi hicho kulipwa ni lazima timu husika ikubaliane na mchezaji mwenyewe.

Kwenye suala la mchezaji kukubali ndipo inaonekana changamoto kwa timu nyingi kwa sababu tayari kuna urafiki mkubwa kati ya Yamal na Williams ambao itakuwa ni rahisi kutumika kama kishawishi cha kumfanya staa huyo akubali kutua Nou Camp.

Katika mahojiano na waandishi wa habari mwaka jana, Williams alithibitisha ukaribu wake na Yamal akisema: “Tunacheka sana. Nadhani ni wazi kuwa tuna tabia sawa au zinazofanana na tunapenda vitu vile vile. Ni kijana ambaye naelewana naye vizuri na kila wakati ninajitahidi kumshauri kadri niwezavyo, kama vile kaka yangu Inaki alivyofanya kwangu.”