Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Davina kashtukia jambo Bongo Movie

Muktasari:

Davina aliyewahi kutamba na tamthilia kupitia runinga, alisema pamoja na kuigiza kwa msanii anatakiwa abuni miradi itakayowaingiza fedha nje ya fani yao ya uigizaji kwa lengo la kuwafanya waendelee kuishi kisupastaa.

MMOJA ya mastaa wakongwe wa filamu nchini, Halima Yahya ’Davina’ mjanja sana, kwani ameshtukia jambo katika tasnia hiyo na kuwashtua wenzake kuwa, imefika wakati wakabuni miradi ya kupiga fedha kijanja.

Davina aliyewahi kutamba na tamthilia kupitia runinga, alisema pamoja na kuigiza kwa msanii anatakiwa abuni miradi itakayowaingiza fedha nje ya fani yao ya uigizaji kwa lengo la kuwafanya waendelee kuishi kisupastaa.

“Kwa sasa kila mtu anatakiwa awe mjasiriamali, yaani kazi kwa kwenda mbele maisha yanaenda kasi mno, ndio maana naendesha shughuli za mgahawa wa chakula ili kuingiza kipato zaidi ya uigizaji, wengine washtuke sasa,” alisema.

Davina alisema mbali na mgahawa huo uliopo Chuo cha Uandishi wa Habari (TSJ), lakini pia ana biashara zake nyingine na amekuwa akiwapata wateja kupitia mgahawa huo na kuwasambazia popote walipo na kuwavutia wengi.