Jack Pentzel anataka kuzaa watoto watatu tu

Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack’
Muktasari:
Jack anaamini idadi hiyo ndiyo anayoweza kuitunza na kuipa elimu bora na hataki kufuata mawazo ya mtu mwingine anayetaka kuzaa watoto wengi au chini ya hao.
STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack’ amesema anataka kuijaza dunia kwa kuzaa watoto watatu tu.
Jack anaamini idadi hiyo ndiyo anayoweza kuitunza na kuipa elimu bora na hataki kufuata mawazo ya mtu mwingine anayetaka kuzaa watoto wengi au chini ya hao.
“Nilijipangia katika maisha yangu nikiingia katika ndoa Mungu anijaalie watoto watatu tu, najua watasoma, wataishi maisha bora na watakuwa na afya njema. Sitaki kuwa na familia nitakayoshindwa kuimudu,”alisema Jack.
Aidha, Jack alisema katika watoto hao watatu hana jinsia anayoipendekeza ila ni wale ambao Mungu ataomjaalia na atakuwa na mapenzi nao bila ya kuwabagua.