Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya kutisha - Sehemu ya 27

MAUAJI 27 Pict

UTANGULIZI

Mkewe Almasi alikuwa amelala chini hatua chache mbele yake. Kichwa chake kilikuwa kimetenganishwa kabisa na kiwiliwili!

“Yesu wangu!” akaguta. Kisha akajisemea:

“Mke wangu naye ameshauawa!”

Aliogopa kuingia ndani zaidi, akatoka nje ya chumba na kufunga mlango.

“Hawa watu wamekuja kumuua mke wangu humu humu ndani!” akaendelea kujisemea huku akipiga hatua za haraka kutoka nje.

SASA ENDELEA


“NI kweli alivyosema yule mganga, mauaji yataendelea. Nilipuuza, sasa yameshatokea” alijiambia wakati akijipakia kwenye gari baada ya kufunga mlango wa nyumba yake.

Aliliondoa gari lakini hakujua alikuwa anakwenda wapi. Akajiuliza anakwenda wapi? Hakupata jibu kichwani mwake. Akaendelea kujiuliza aende polisi au aende kwa mchngaji wake au aende kwa Maria.

Kama ni kwa mchungaji asingeweza kwenda  kwa sababu alikuwa amelewa.

Kadhalika asingeweza kwenda polisi kwa sababu aliona kusingekuwa na msaada wowote. Polisi hao wangefika nyumbani kwake na kumhoji maswali na kisha kuondoka  na mwili wa mke wake.

Akaona bora aende kwa Maria. Kama ni kwenda polisi atakwenda baada ya kutoka kwa Maria.

Alifika Tegeta alikokuwa akiishi Maria.

Maria alishangaa alipomuona shemeji yake akiwasili nyumbani kwake usiku ule.

“Karibu shemeji, mbona umekuja usiku huu?”

“Dada yako ameshachinjwa sasa hivi” akamwambia.

Maria alishituka sana.

“Dada yangu yupi aliyechinjwa?”

“Leo humjui dada yako, kwani yule uliyempeleka kwa mganga ni nani wako?”

“Shemeji usiniambie, dada  yangu nayeye amechinjwa!”

“Amechinjwa sasa hivi…”

“Hebu nieleze imekuwaje?’

Almasi akamueleza tukio zima lilivyotokea.

“Sasa huoni kwamba hao si watu wa kawaida, wameingiaje humo ndani  na wametokaje?”

“Walivyoingia  sijui lakini hawajatoka. Nimefunga milango yote. Nilisikia wakimuuliza kama yeye ni mke wa Almasi. Alipowajibu ndiyo, nikasikia wakimwambia mume wako alikuweka dhamana na wewe umeshindwa kutimiza masharti ya dhamana halafu wakamchinja”

“Wewe ulikataa bure kwenda kwa mganga, sasa unaona. Yule mganga alituambia mauaji yataendelea”

Almasi alitikisa kichwa kusikitika.

“Ni kweli nilifannya kosa. Ninahisi  mimi ndiye nitakayekuwa wa mwisho  kuuawa”

“Yule  mganga alituambia mauaji yataendelea”

“Sasa nipeleke sasa hivi kabla sijauawa”

“Subiri kwanza. Kwani umeshatoa ripoti polisi”

“Sijatoa  ripoti polisi. Nimekuja  huku kwanza”

“Sasa kwanini  hukutoa ripoti  polisi wakati mke wako ameuawa?”

“Nimeona hawanisaidii. Bora nianze na mahali nitakapopata msaada wa maisha yangu”

“Ukumbuke  umesema kwamba hao watu umewafungia ndani”

“Nikitoka hapa ndio nitakwenda polisi. Kama hao watu wamo watatolewa na polisi”

“Haya subiri twende kwa huyo mganga”

Dakika chache baadaye Almasi na shemeji yake wakawa njiani kuelekea kwa huyo  mganga aliyekuwa akiishi  mbali kidogo na mtaa aliokuwa akiishi Maria.

“Lile tukio limenishitua sana. Wale ndio watu waliowaua wanangu na leo wamemuua mke wangu. Nimewasikia waziwazi. Maneno yao  ni yale yale waliyokuwa wakiwaambia wanangu  kabla  ya kuwaua.  Sasa sijui  kama wale ni binaadamu au ni mashetani?”

“Kwani wewe hukumbuki kama uliwahi  kuweka nadhiri?”

“Sijaweka nadhiri mahali popote. Halafu mimi sina tabia ya  kupenda ushirikina. Nilishampokea Yesu siku nyingi”

“Yule mganga alisema uliweka nadhiri”

“Sasa acha nikamsikilize mwenyewe”

“Kama shemeji ungekubali mapema, haya matatizo yasingetokea”

Almasi akanyamaza kimya. Maneno ya Maria yalikuwa yakimchoma moyo. Kimoyomoyo alikiri  kwamba alifanya kosa kutokukubali alipoambiwa aende kwa mganga.

Kichwani kwake alikuwa akijiuliza kama aliwahi kwenda  kwa mganga angalau mara moja na kuweka nadhiri aliyoambiwa. Akili yake ilikataa kabisa.

Walipofika nyumbani kwa mganga walibisha na kuingia ndani. Aliyewakaribisha alikuwa ni mganga mwenyewe.

“Karibuni” Mganga aliwambia akiwa amemkumbuka Maria.

Wakiwa wameketi katika chumba cha uganga, Maria akamwambia mganga.

“Nadhani unakumbuka tulivyokuja  kwako na mwenzangu?”

“Nawakumbuka vizuri”

“Ulituambia kwamba mauaji yataendelea na kweli huu usiku dada  yangu ameuawa usiku huu katika mazingira  yale yale”

Mganga akashituka kidogo.

“Dada yako yule yule uliyekuja naye?” akauliza kwa fadhaa kisha akaongeza.

“Niliwambia mje na mume wale lakini sikuwaona tena”

“Mume wake ndiye huyu  niliyenaye”

“Kwanini bwana  umechelewa  kuja kwangu mpaka  matatatizo yanazidi kutokea?” Mganga akamuuliza Almasi.

“Tatizo lililonizuia ni kwamba nilikuwa najaribu kujiuliza niliweka nadhiri wapi lakini sikupata jibu”

“Uliweka nadhiri. Jaribu kukumbuka sana”

“Labda  kama wewe unaijua nikumbushe”

“Miaka kadhaa nyuma ulikuwa masikini sana, ulipata wapi mali yako na kwa njia ipi?”

Almasi alipotajiwa mali, mawazo yake yakaenda mbali sana. Kumbukumbu zikaanza kumjia.

Ilikuwa ni mwaka 2001 alipomuacha mke  wake pamoja na  watoto wake waliokuwa wamezaliwa wakati huo na kuelekea Marerani kwenda kuchimba madini.

Baada ya kufika huko, Almasi ambaye jina lake halisi lilikuwa Amon Marwa kabla ya kujibatiza jina la Almasi aligundua kuwa shughuli nzima ilikuwa imetawaliwa na ushirikina mtupu. Alipata mtu aliyemshauri kwamba ili apate uhakika  wa mafanikio nilazima aende kwa mganga.

Akapelekwa kwa mganga mmoja aliyekuwa Korogwe. Mganga alipomsikiliza, alimwambia Amon ili apate madini ya kumpa utajiri ni lazima atoe kafara la roho.

Amon akagutuka.

“Kafara la roho? Kafara la roho ndio kitu  gani?”

“Umtoe mtu kafara”

“Kivipi?”

“Hujui kutoa mtu kafara, ndiyo  umeanza sasa kazi ya kuchimba madini?”

“Nimeanza muda kidogo lakini sijapata mafanikio. Watu wameniambia nijaribu kwenda kwa waganga”

“Kuna makafara yanayotolewa na baadhi ya watu kwenye machimbo”

“Nilivyosikia ni kwamba watu wanatoa makafara ya wanyama kama mbuzi”

“Sasa ili wewe upate utajiri unaoutaka ni lazima utoe kafara la roho ya mtu”

“Ndiyo nilikuwa  nataka ufafanuzi, kafara hilo linatolewa vipi?”

“Uchinje mtu kwenye chimbo lako!”

“Mama yangu…!”

“Kama uko tayari na una uhakika wa kupata mtu wa kumtoa kafara, sema nikupe msaidizi wangu uende naye akakufanyie kazi yako”

Amon  baada  ya kuwaza kidogo alimuuliza mganga huyo.

“Kama tutatoa kafara la mtu, ndiyo itakuwaje?”

“Utapata mali itakayokupa utajiri katika masiha yako yote.Lakini ni endapo utafuata masharti yangu”

“Masharti gani hayo?”

“Sharti la kwanza, ukishapata  mali mara moja tu usirudi tena Marerani. Sharti la pili, kila mwakalazima ukamwage baharini sarafu zenye thamani ya robo ya utajiri  wako, yaani unawapa sadaka majini waliokupautajiri huo”

“Kama nimekuelewa vizuri, sharti  la kwanza nikishatoa mtu  kafara na kufanikiwa kupata mali niondoke Marerani na nisirudi tena. Na sharti la pili, kila  mwaka nitoe sarafu zenye thamani ya robo ya utajiri wangu, si ndiyo”

“Ndiyo hivyo”

“Sasa mimi nina maswali”

“Uliza”

“Kwanza  nataka  kujua ina  maana hayo madini nitakayopata baada ya kutoa  hilo kafara, ndiyo yatakayonipa  utajiri maishayangu yote?”

“Sawali zuri sana. Utapata utajiri ambao utauendeleza kwa biashara nyingine”

“Na hizo sarafu ambazo unasema nikamwage baharini kila mwaka nitazipata  wapi?”

“Unatakiwa uweke kidogo kidogo kwa mwaka mzima, zikifikia robo ya utajiri ulionao, unazifunga katika vifurshi saba vya kitambaa cha rangi nyeupe kisha unakodiboti na kwenda kuzitosa baharini”

“Yaani nifanye hivyo hadi kufa kwangu”

“Ndiyo, usiache. Wale majini waliokupa madini nao wanataka sadaka zao”

“Kama una uhakika kuwa nitapata utajiri, naweza kufanya hivyo lakini nitampata wapi huyo mtu wa kumtoakafara”

“Mtu yeyote tu”

“Sasa nitampataje?”

“Unatuma watu wakutafutie mtu ambaye watamfunga kamba na kumpeleka kwenye lile chimbo wakati wa usiku kisha atachinjwa pale na mwili wake utakwenda kuzikwa”

“Hapo panataka kazi. Kumkamata mtu na kumfunga…!”

“Mbona ni jambolinalowezekana. Yule mtu anakamatwa usku vichochoroni. Kama mna gari, mnampakia na kumpeleka kunakohusika”

“Wakati huo wewe utakuwa wapi?’

“Chukua namba yangu ya simu. Siku ukiona una  mpango wa  kupata mtu unaniagiza ninakuja siku hiyo hiyo au ninatuma mtu wangu. Hiyo kazi inafanyika usiku wa manani”

“Sawa. Nipe namba yako”

Mganga alimpa Amon namba yake ya simu na Amon akampa mganga huyo namba yake.

“Sasa  wewe nenda, siku yoyote ukiona una mpango wa kupata mtu nipigie simu”

“Sawa. Sasa utakapoifanya hiyo kazi utahitaji kiasi gani?”

“Hii kazi ni kubwa na kima changu ni shilingi milioni  mojananusu”

“Mbona ni kiasi kikubwa sana?”

“Ndiyo kima changu na ni kwa sababu nina uhakika kwamba utapata utajiri kwani wengi wamefanikiwa.”


“Naona una uhakika na kazi yako. Nitakutafutia hiyo pesa kisha  nitakupigia simu kukujulisha kama nimepata mtu”


“Sawa”