Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bab'kubwa... Hivi ndivyo Tanzania Open ilivyofunika Arachuga

Arusha Pict
Arusha Pict

Muktasari:

  • Snow anayeichezea klabu ya Muthaiga, alionyesha kiwango cha hali ya juu kwa kupata jumla ya mikwaju 186 na kuwashinda wacheza gofu zaidi ya 200 kutoka mataifa mbalimbali walioshiriki katika mashindano hayo.

MCHEZA gofu nyota wa Kenya, Greg Snow ameendeleza wimbi la ushindi kwa nchi hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open, yaliyomalizika wiki iliyopita katika Uwanja wa Gofu wa Kili, mkoani Arusha.

Snow anayeichezea klabu ya Muthaiga, alionyesha kiwango cha hali ya juu kwa kupata jumla ya mikwaju 186 na kuwashinda wacheza gofu zaidi ya 200 kutoka mataifa mbalimbali walioshiriki katika mashindano hayo.

Ushindi wa Snow umeifanya nchi hiyo kuweka historia ya kutwaa mara mbili mfululizo baada ya mwaka jana mchezaji Daniel Nduva wa klabu ya Nyali kutwaa ubingwa huo.

Mashindano hayo, yaliyoandaliwa na Chama cha Gofu Tanzania (TGU), yalikuwa na ushindani na msisimko mkubwa na wachezaji wa kigeni walitawala.

Mchezaji kutoka Rwanda, Celestin Nsanzuwera aliibuka mshindi wa pili baada ya kupata mikwaju 294, huku Mkenya, Dainel Nduva  akifungana na Mtanzania Isaac Wanyeche waliomaliza nafasi ya tatu baada ya kupata  mikwaju 295 kila mmoja.

Nafasi ya nne na tano zilichukuliwa na Wakenya Mike Kisia na Justus Madoya waliopata mikwaju 297 na 299 mtawalia.

Mambo hayakuwa mazuri kwa mcheza gofu maarufu wa Tanzania, Nuru Mollel na kujikuta wakimaliza nafasi ya 12 kwa kupata mikwaju 308.

AR05

Katika mashindano ya mwaka jana, Mollel alimaliza nafasi ya pili, nyuma ya Nduva kwa tofauti ya mkwaju mmoja.

Kwa upande wa wachezaji wa ridhaa, Kenya ilitawala tena na Sammy Mulama alipata mikwaju 304 katika mashindano hayo ya mashimo 72, huku nafasi ya pili ilichukuliwa na Mkenya Josphat Rono kwa mikwaju 308 na Mtanzania Isiaka Daudi alimaliza wa tatu kwa kupata mikwaju 310.

Washindi walikabidhiwa vikombe na zawadi za fedha taslimu zilizotolewa na mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa Sheria wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Agapinus Tax ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa mashindano hayo.


AR01

MAFANIKIO MAKUBWA

Tax aliwapongeza washindi na washiriki wote kwa kujituma na kuhakikisha mashindano yanakuwa ya kusisimua.

“Mashindano haya hayajaonyesha tu vipaji vya kipekee, bali pia yameangazia nguvu ya kuunganisha michezo barani Afrika. Vodacom Tanzania Open 2024 imedhihirisha uwezo wa nchi yetu kuandaa matukio ya kiwango cha kimataifa,” alisema Tax.

Tax aliongeza, tukio hilo limechangia pakubwa katika sekta ya utalii na ushirikiano wa kijamii, hasa katika Jiji la Arusha.

“Matukio kama haya yanaimarisha uchumi wa ndani na kukuza michezo kama nyenzo ya maendeleo ya kitaifa. Vodacom Tanzania tunajivunia kuunga mkono juhudi zinazoinua mchezo wa gofu na kuimarisha mshikamano wa kijamii,” alisema.


AR02

USHIRIKI KIMATAIFA

Mbali ya Kenya, Rwanda na Tanzania, mashindano hayo pia yalishirikisha wachezaji gofu kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Afrika Kusini, Malawi, Zimbabwe na Uingereza.

Hali hii imeonyesha jinsi mashindano ya Vodacom Tanzania Open yalivyoifungua Tanzania na kuwavutia wachezaji mbalimbali wa kimataifa.

Mbali ya lengo la kushindana na kutwaa ubingwa, wachezaji hao pia wamekuja kuongeza nafasi ya kupanda viwango (ranking) kwani washindi wa mashindao ya Vodacom Tanzania Open wanaingia katika orodha ya viwango vya dunia The World Amateur Golf Rankings (WAGR).

Mwenyekiti wa TGU, Gilman Kisiga alitumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wadhamini wote waliosaidia kufanikisha tukio hilo. “Mashindano haya ni ushahidi wa ukuaji wa mchezo wa gofu nchini mwetu. Tunawashukuru kwa dhati washirika wetu, hasa Vodacom Tanzania, kwa msaada wao usioyumba katika kukuza mchezo huu,” alisema Kisiga.


AR03

MANUFAA KITALII

Mashindano haya pia yameleta mwamko mkubwa katika sekta ya utalii. Kwa mujibu wa Tax, Arusha imefaidika pakubwa kutokana na idadi kubwa ya wageni waliotembelea jiji hilo kwa ajili ya mashindano haya.

Tukio hili limeonyesha jinsi michezo inavyoweza kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi, huku pia likisaidia kujenga jina la Tanzania kimataifa.

“Kupitia mashindano haya, tunaendelea kuimarisha nafasi yetu kama taifa lenye uwezo wa kuandaa matukio makubwa ya kimichezo. Tunaamini mchezo wa gofu utaendelea kukua na kuleta faida kwa jamii nzima,” alisema Tax.


AR04

KIZAZI KIPYA

Kisiga alisisitiza lengo la TGU ni kutumia mashindano kama haya kuhamasisha kizazi kipya cha wachezaji wa gofu.

“Pamoja, tunaendelea kujenga jukwaa linalochochea kizazi kipya cha wacheza gofu na kuitangaza Tanzania kama eneo bora la michezo ya hali ya juu,” aliongeza.

Kwa jumla, mashindano hayo ya Tanzania Open 2024 sio tu yameonyesha vipaji vya wachezaji wa ndani na nje ya nchi, bali pia yameonyesha jinsi ushirikiano kati ya sekta ya michezo na wadhamini unavyoweza kuleta matokeo mazuri kwa taifa.

Mashindano haya yanaacha alama kubwa katika historia ya mchezo wa gofu nchini na yanatoa mwanga wa mustakabali wa michezo kama chombo cha maendeleo na mshikamano.