Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyu ndiye 'MK14' anayezeeka na utamu wake

MEDDIE Pict

Muktasari:

  • Oktoba 10, Kagere aliyezaliwa mwaka 1986 huko Uganda ila akiitumikia timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, anatimiza miaka 39, huku kwa mujibu wa wikipedia ametimiza miaka 21, tangu aanze kucheza soka 2004 akiwa na Mbale Heroes FC ya Uganda.

UNAPOTAJA nyota wa kigeni waliofanya vizuri na kujiwekea rekodi za kipekee, hutoacha kumtaja mshambuliaji wa zamani wa timu za Simba, Singida Big Stars na sasa Namungo FC, Meddie Kagere ‘MK14’, kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao.

Oktoba 10, Kagere aliyezaliwa mwaka 1986 huko Uganda ila akiitumikia timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, anatimiza miaka 39, huku kwa mujibu wa wikipedia ametimiza miaka 21, tangu aanze kucheza soka 2004 akiwa na Mbale Heroes FC ya Uganda.

Licha ya umahiri wa nyota huyo aliyetamba na timu mbalimbali zikiwamo Gor Mahia, Simba, ATRACO FC, Kiyovu Sports, Police FC na Rayon Sports, ni wazi enzi zake za kiuchezaji zinakaribia kufikia tamati kama ambavyo Mwanaspoti linavyomuelezea.


MED 01

UMRI

Waswahili husema umri ni namba tu ingawa kuna maeneo hasa ya mchezaji anapofikia huwa sio hiari tena bali humlazimisha kuangalia namna nyingine ya kufanya, hali ambayo kwa sasa inamkuta Kagere ya kushindwa kuendana na kasi ya kiushindani.

Kwa eneo la ushambuliaji ambalo hutumia nguvu zaidi, ni wazi Kagere anapishana nalo kutokana na umri alionao hali inayochangia pia kumuona akiendelea kupata wakati mgumu wa kucheza kikosi cha kwanza mara kwa mara akiwa na Namungo FC.

Mshambuliaji kwa sasa anayeishangaza dunia ni Kazuyoshi Miura ‘King Kazu’ anayeichezea Atletico Suzuka ya Ligi Kuu ya Japan, aliyeweka rekodi ya mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kucheza soka ambapo Februari mwaka huu ametimiza miaka 58.

Kazuyoshi anacheza kwa msimu wake wa 39 kwenye soka kwa sasa akiwa anawashangaza wengi kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akipambana na wachezaji wenye umri mdogo uwanjani, huku taarifa zikidai aliocheza nao akiwa na miaka 19, wameshastaafu.

MED 05

Nyota huyo alianza kucheza soka la ushindani mwaka 1986, akiitumikia Santos ya Brazil, ikiwa ni klabu iliyomuibua staa mkubwa duniani Pele, aliyoichezea misimu minne na kurudi Japan na kutwaa tuzo ya MVP mwaka 1993, akiwa na Tokyo Verdy.

Baadhi yao ambao wanacheza baada ya kufikisha miaka 40 lakini hawajafikia rekodi ya Kazuyoshi ni pamoja na staa wa Peru Paolo Guerrero (aliyefikisha miaka 41, Januari mwaka huu) na nyota wa timu ya taifa ya Paraguay, Roque Santa Cruz (43).

Wengine ni Mbrazil Felipe Melo (41) na mshindi wa Ballon d’Or mara tano, Cristiano Ronaldo aliyefikisha pia 40, Februari mwaka huu, huku akitamba na timu za Manchester United na Real Madrid japo kwa sasa anaichezea Al Nassr ya Saudi Arabia.

Ni wachezaji wachache wenye uwezo wa kujitunza na kucheza soka kwa muda mrefu kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa timu ya Simba na Taifa Stars, Madaraka Selemani ‘Mzee wa Kiminyio’, aliyecheza na kustaafu akiwa na miaka 42.


MED 02

SOKA LA KISASA

Katika soka la kisasa, makocha wengi wanapenda kutumia washambuliaji wanaocheza nafasi zaidi ya moja katika eneo lote la mbele kwa maana awe na uwezo wa kufunga, lakini wakati huohuo azuie mashambulizi ya wapinzani kuanzia langoni mwao pia.

Kagere sio mshambuliaji anayeendana na mabadiliko hayo kwani mara nyingi amezoea kubaki mbele na kusubiri kuletewa mipira jambo linalomfanya kuzidi kupigwa bao na vijana wadogo wanaoweza pia kushambuliaji wakitokea maeneo tofauti ya uwanjani.

Kuonyesha taratibu nyota huyu anatoka katika mfumo, Januari mwaka huu viongozi wa Namungo FC wakaamua kumfuata aliyekuwa mshambuliaji wa KenGold, Joshua Ibrahim ili kuendana na mabadiliko ya kiuchezaji ya kocha wa kikosi hicho, Juma Mgunda.

Ibrahim aliyejiunga na KenGold aliyoifungia mabao manne ya Ligi Kuu mwanzoni mwa msimu huu akitokea Tusker FC ya Kenya, amejiunga na Namungo FC kwa mkopo ingawa tayari ameingia moja kwa moja katika kikosi, huku akiwa mshambuliaji tegemeo.

Tangu ajiunge na ‘Wauaji wa Kusini’, Joshua ameifungia bao moja la Ligi Kuu Bara na kufikisha matano, wakati iliposhinda 1-0, ugenini dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons Februari 14, 2025, huku Kagere akitimiza mwaka mzima bila ya kufunga.


MED 03

REKODI TAMU

Nyota huyo raia wa Rwanda wakati anaondoka Msimbazi aliweka rekodi tamu kwa mastaa wa kigeni katika Ligi Kuu Bara ambayo imeendelea kuishi hadi leo, kwani licha ya wachezaji wengi waliokuwa bora na wazoefu kucheza  wameshindwa kuifikia.

Kagere alitua Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya msimu wa 2018-2019 na kufunga mabao 23 na kuipiku rekodi ya aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ya wachezaji wa kigeni kufunga mabao mengi msimu mmoja alipofunga 21 msimu wa 2015-2016.

Msimu wa pili kwa staa huyo akiwa na Simba pia, alifunga mabao 22 na kutetea tuzo ya mfungaji bora ikiwa pia ni rekodi kwani, haikuwahi kutokea kwa mchezaji yeyote iwe mzawa au wa kigeni kutwaa tuzo ya ufungaji bora mara mbili mfululizo.

MED 04

Nyota wengine waliotwaa tuzo ya mfungaji bora japo kwa msimu tofauti tangu mwaka 2000 ni Simon Msuva, Amissi Tambwe na John Bocco.

Bocco alitwaa msimu wa 2011-2012 enzi akiwa na Azam FC alipofunga mabao 19, akairudia tena 2020-2021 alipokuwa na Simba akifunga 16 huku Tambwe akiichukua 2013-2014 na Simba alipofunga 19, kisha akaichukua alipokuwa Yanga 2015-2016 akifunga 21.

Kwa upande wa Simon Msuva alichukua tuzo hiyo akiwa na Yanga akifanya hivyo msimu wa 2014-2015 alipofunga mabao 17 kisha akairudia tena msimu wa 2016-2017, wakati alipofunga 14 sambamba na aliyekuwa nyota wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa.

Baada ya hapo ‘MK14’ akaachana na kikosi cha Simba na kujiunga na Singida Big Stars msimu wa 2022-2023 ambapo aliendelea kuonyesha kiwango bora kufuatia kufunga mabao manane, kisha msimu uliopita akaichezea Namungo na kufunga mabao mawili.

Licha ya rekodi hizo tamu ila kwa sasa nyota huyo anaandamwa na ukame wa mabao kwani mchezo wa mwisho kufunga bao ni ule wa Februari 24, 2024, dhidi ya KMC FC, ambao kikosi hicho cha ‘Wauaji wa Kusini’ kikiwa ugenini kilitoka sare ya 2-2.

Ni wazi ile nguvu na kasi yake imepungua kwa kiasi kikubwa jambo linalomfanya kupitia kipindi kigumu cha kutocheza mara kwa mara kikosi cha kwanza, ingawa hakuna ubishi ni moja ya washambuliaji wazuri wanaojua kucheka na nyavu za wapinzani.