Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SHANGAZI IVA: Kaongoza soka, halafu ukocha timu ya taifa

Muktasari:

  • Kwa kiasi kikubwa mafanikio ya nchi hiyo yanatokana na wanawake kuwa mstari wa mbele hata katika kufundisha na kuongoza timu ya taifa ya wanaume na miongoni mwa wanawake viongozi waliotoa mchango mkubwa wa mafunzo na ushauri ulioifanya Croatia kupanda daraja la umaarufu ni Shangazi Iva.

Croatia ambayo ni moja ya nchi ndogo za la Bara la Ulaya iliyojitenga na Shirikisho la Yugoslavia 1991 imepata mafaniko makubwa katika kandanda katika miaka ya karibuni na kusababisha kuandika historia ya aina yake na hasa kwa wanawake kuwa mstari wa mbele kufundisha na kuongoza timu na shirikisho la kandanda la nchi.

Kwa kiasi kikubwa mafanikio ya nchi hiyo yanatokana na wanawake kuwa mstari wa mbele hata katika kufundisha na kuongoza timu ya taifa ya wanaume na miongoni mwa wanawake viongozi waliotoa mchango mkubwa wa mafunzo na ushauri ulioifanya Croatia kupanda daraja la umaarufu ni Shangazi Iva.

Mwanamama huyo ambaye sasa ana miaka 56, kwa mwaka wa saba sasa huwa hakosekani katika ubao wa viongozi wa vikosi vya kadanda vya wanaume na wanawake vya Croatia. Alikuwa mmoja wa washauri wa kikosi cha Croatia kilichofungwa 4-2 na Ufaransa katika fainali ya Kombe la Dunia Russia 2018.

Katika michuano ile ya Russia shangazi aliungwa mkono kwa kuwa karibu na wachezaji na aliyekuwa Rais wa Croatia, mwanamama Kolinda Grabar-Kitarović.

Nchini Croatia, nchi yenye watu milioni 4.2 (wanawake milioni 2.3), jina la kwanza la zaidi ya asilimia 10 ya wanawake ni Iva, lakini ukimsikia mtu anamtaja Shangazi Iva, basi si mwingine isipokuwa ni Iva Olivari maarufu kama Shangazi Iva aliyekuwa mmoja wa wanamichezo mashuhuri wa Croatia na pia alitamba katika tenisi tangu akiwa mdogo na kuwa bingwa wa mchezo huo kwa wachezaji wa chini ya umri wa miaka 14.

Aliacha kucheza tenisi kutokana na maumivu na kuanza kazi katika Shirikikisho la Kandanda la Croatia huku akichukua mafunzo ya ukocha wa soka. Mwaka 2012 pale mchezaji mashuhuri wa Croatia, Davor Suker alipoacha kuwa kocha wa timu ya taifa ya Croatia na kuwa rais wa Shirikisho la Kandanda la Croatia, alimkabidhi Iva mikoba ya ukocha wa timu ya taifa.

Kilichowashangaza wengi ni kwamba licha ya kwenda vizuri na timu hiyo zilipofanyika fanali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil, alitafutwa mwanamume kuchukua nafasi yake, huyu akiitwa Igor Stimac. Iva ambaye ndiye aliyeiongoza timu hiyo hadi kukata tiketi ya kucheza fainali hizo hakutakiwa hata kukaa na wachezaji na viongozi wa timu hiyo.

Lakini, alikwenda Brazil kama mtazamaji na badala ya kuwatembelea wachezaji wa Crotia hotelini wao walimfuata katika hoteli aliyofikia. Huo ulikuwa mpango mchafu na mfumo dume kwa vile baada ya kuifikisha Croatia katika fainali za Kombe la Dunia ilionekana ni kocha mwanamume ndiye angefaa kumaliza kazi iliyobaki.

Baada ya Coatia kuongozwa na mwanamama ambaye pia ni mwanamichezo, Rais Kolinda Grabar-Kitarovic na viongozi wa soka walijikuta hawawezi kumbadilisha kocha wakati timu ilipofanya safari ya Russia kushiki fainali za Kombe la Dunia.

Wakati akicheza tenisi alikuwa mmoja wa wachezaji mashuhuri wa mchezo huu duniani na aliwahi kumshinda mchezaji namba moja duniani wa wakati ule, Steffi Graf wa Ujeumani.

Katika mahojiano ya hivi karibuni, Iva alisema anafurahia namna ambavyo wachezaji wanavyomheshimu na wakati watu wengi wa Croatia humwita Shangazi, wachezaji wanamwita darling (mpenzi).

"Wanayo haki ya kuniita mpenzi maana tunapendana," alisema Iva katika mahojiano hayo.

Lakini, ukiachilia mbali Croatia kuwa nchi ambayo timu yake ya taifa ya kandanda kuwahi kuwa chini ya kocha mwanamke, jambo lingine la ajabu ni kwamba wengi wa viongozi wa Shrikisho la Kandanda la Croatia ni wanawake.

Shangazi Iva anasema ni matumaini yake watajitokeza wanawake wengine nchini humo kuwa makocha wa kandanda wa klabu mashuhuri za nchi hiyo na baadaye Croatia itakuwa na kocha mwanamke kama alivyokuwa yeye miaka michache iliyopita.

Fikiria hali itakuwaje hapa kwetu ikitokea mwanamke kuchaguliwa kuwa kocha wa Taifa Stars na kiongozi mkuu wa kikosi kama ilivyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama? Nakuachia msomaji ufikirie na kama hupati jibu waulize rafiki zako.